Pata taarifa kuu

Vita nchini Ukraine: Biden akaribisha ukakamavu wa Kyiv na kuapa kwamba 'Putin atapoteza'

Marekani imeendelea kuonyesha uungaji wake mkono kwa Ukraine. Joe Biden amesema Jumanne Februari 21 kwamba Ukraine inaendelea kuwa 'huru', wakati wa ziara yake nhini Poland, kabla ya kumbukumbu ya kwanza ya uvamizi wa Urusi nchini Ukraine. 

Rais Joe Biden atoa hotuba kuadhimisha mwaka mmoja wa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Jumanne, Feb. 21, 2023, katika bustani ya Royal Castle huko Warsaw.
Rais Joe Biden atoa hotuba kuadhimisha mwaka mmoja wa uvamizi wa Urusi nchini Ukraine, Jumanne, Feb. 21, 2023, katika bustani ya Royal Castle huko Warsaw. AP - Evan Vucci
Matangazo ya kibiashara

"Kiev ina nguvu, Kiev ni jasiri, imesimama kidete na zaidi ya yote iko huru," rais wa Marekani ameuambia umati uliokusanyika nje ya Jumba la Kifalme huko Warsaw, katika hotuba yake huko Poland muda mfupi kabla ya kumbukumbu ya kwanza ya mwanzo wa uvamizi wa Urusi.

Joe Biden pia amesema uungwaji mkono kwa Ukraine "hautapungua". "Hatupaswi kuwa na shaka: msaada wetu kwa Ukraine hautadhoofika, NATO haitagawanyika na hatutaachilia", amesemarais wa Marekani. Nchi za Magharibi "hazina njama ya kushambulia Urusi", pia amebaini Joe Biden. "Nchi za Magharibi hazijapanga njama ya kushambulia Urusi, kama Putin alivyosema leo. Mamilioni ya raia wa Urusi ambao wanataka tu kuishi kwa amani na majirani zao sio adui,” alihoji rais huyo wa Marekani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.