Pata taarifa kuu

Joe Biden ziarani Kyiv: Marekani yaahidi kuisadia Kyiv kushinda vita vya Urusi

Alitarajiwa nchini Poland, na hatimaye alitua Kyiv Jumatatu hii, Februari 20 asubuhi. Ziara ya kushtukiza ya Joe Biden nchini Ukraine. Rais wa Marekani alikuja kuihakikishia nchi hii uungaji mkono wa Marekani dhidi ya uvamizi wa Urusi. Ishara ya nguvu.

Rais wa Marekani Joe Biden, akiwa na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky, mbele ya monasteri ya Saint-Michel-au-Dôme-d'Or, mjini Kiev, Jumatatu hii, Februari 20, 2023.
Rais wa Marekani Joe Biden, akiwa na mwenzake wa Ukraine Volodymyr Zelensky, mbele ya monasteri ya Saint-Michel-au-Dôme-d'Or, mjini Kiev, Jumatatu hii, Februari 20, 2023. AP - Evan Vucci
Matangazo ya kibiashara

Karibu mwaka mmoja baada ya Urusi kuanza chokochoko zake dhidi ya Ukraine, ujumbe wa rais wa Marekani ni rahisi, uliofupishwa kwa maneno machache: "Kyiv inajizatiti, Ukraine inajizatiti, demokrasia iko imara. Marekani na dunia zinaunga mkono Ukraine,” kwa muda mrefu iwezekanavyo.

Na ili kuambatanisha vitendo na maneno, Joe Biden alitangaza awamu ya msaada mpya wa kijeshi kwa nusu ya dola bilioni moja. Msaada huu utahusu hasa vifaru, na vifaa mbalimali vya kijeshi ikiwa ni pamoja na risasi na makombora.

Ujumbe kwa Ukraine, lakini pia kwa Shirikisho la Urusi. Vikwazo vipya dhidi ya vyombo vinavyochochea vita vya Urusi vitatangazwa katika siku zijazo.

Hata hivyo, Moscow ilionywa saa chache kabla ya ziara hii mapema Ijumaa jioni. Inakuja saa chache kabla ya hotuba ya Vladimir Putin kuadhimisha mwaka wa kwanza wa kile Warusi bado wanaita "operesheni maalum ya kijeshi".

Ujumbe huo pia ni kwa Wamarekani, ambao uungaji mkono wao kwa Ukraine unaanza kudhoofika kwa maoni ya umma kulingana na baadhi ya tafiti. Ili kuwaonyesha haya yote ni kwa nini yanafanyika.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.