Pata taarifa kuu

China inapanga kuihami Urusi: Marekani

NAIROBI – Waziri wa Mambo ya nje wa Marekani Antony Blinken amesema China inapanga kuipa Urusi, silaha za kuishambulia Ukraine.

Kiongoiz wa China Xi Jiping
Kiongoiz wa China Xi Jiping AFP - -
Matangazo ya kibiashara

Blinken ameimbia Televisheni ya CBS news iwapo China itatekeleza mpango wake, itachochea zaidi vita hivyo na ni kauli anayoitoa baada ya kukutana na mwanadiplomasia wa China Wang Yi, wakati wa mkutano kuhusu usalama mjini Munich mwishoni mwa wiki iliyopita.

“Tuna wasiwasi kuwa huenda China inampango wa kuisaidia Urusi kuendelea kutekeleza uvamizi wake nchini Ukraine.”ameeleza Antony Blinken.

China ambayo ni mshirika wa karibu wa Urusi, inakanusha madai hayo ya Marekani na kusema haigemei upande wowote kwenye vita vinavyotimiza mwaka mmoja siku ya Ijumaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.