Pata taarifa kuu
USHIRIKIANO-DIPLOMASIA

Joe Biden afanya ziara ya kushtukiza Kyiv

Rais wa Marekani Joe Biden amefanya ziara ya kushtukiza mjini Kyiv siku ya Jumatatu, akiahidi silaha mpya na msaada 'usiotetereka' kwa mshirika wake wa Ukraine, siku chache kabla ya maadhimisho ya mwaka wa kwanza wa uvamizi wa Urusi.

Rais wa Marekani Joe Biden na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ziara ya rais wa Marekani huko Kyiv mnamo Februari 20, 2023.
Rais wa Marekani Joe Biden na Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky ziara ya rais wa Marekani huko Kyiv mnamo Februari 20, 2023. AFP - DIMITAR DILKOFF
Matangazo ya kibiashara

"Nitatangaza kuipa Ukraine vifaa vingine muhimu, ikiwa ni pamoja na vifaa vya kijeshi, mifumo ya kupambana na silaha nzito na rada za uchunguzi wa anga," rais wa Marekani amemhakikishia mwezake wa Ukraine, kulingana na taarifa kutoka Ikulu ya White, kwa ziara yake ya kwanza nchini Ukraine.

Wakati wa mkutano na waandishi wa habari na Rais Volodymyr Zelensky, ametaja dola milioni 500 za msaada wa mpya, maelezo ambayo yatatangazwa katika siku zijazo. "Ninafikiri ni muhimu kwamba kusiwe na shaka kuhusu uungwaji mkono wa Marekani kwa Ukraine," amesema tena kuhusu ziara yake katika mji mkuu wa Ukraine.

Ukraine inahitaji silaha na makombora ya masafa marefu kwa silaha zake nzito na vifaru ili kukabiliana na mashambulizi mapya ya Urusi na kuanzisha mashambulizi yake yenyewe na kutwaa tena maeneo yanayokaliwa na jeshi la Moscow Mashariki na Kusini.

Ziara hii ya kwanza Bw. Biden nchini Ukraine inafuatia zile za viongozi wengi wa Ulaya katika mji mkuu wa Ukraine na ile ya Bw. Zelensky mjini Washington mwezi Desemba mwaka jana.

Bw Zelensky ameipongeza ziara hii kama "ishara muhimu ya uungwaji mkono". Pia amewaambia waandishi wa habari, pamoja na rais wa Marekani, kwamba wawili walitaka kujadili "jinsi ya kushinda (vita) mwaka huu". Ameongeza, msaada wa kijeshi wa Marekani kwa Ukraine unaonyesha kuwa Urusi "haina nafasi ya kushinda" vita.

Tahadhari za mfumo wa ulinzi wa anga pia zimesikika Jumatatu wakati wa ziara ya rais wa Marekani, wamebaini waandishi wa habari wa shirika la habari la AFP. Joe Biden alikuwa na Rais Zelensky, wakitoka katika kanisa ambalo walikuwa wamekaa kwa dakika chache, wakati ving'ora vilipolia, bila kusababisha hofu. Rais wa Marekani pia ameonyesha kuvutiwa kwake na ujasiri wa Waukraine mbele ya mvamizi. "Ni zaidi ya kishujaa," amesema.

Ziara ya rais wa Marekani inajiri huku Ukraine ikikabiliwa na mapigano yanayozidi kuongezeka mashariki mwa nchi hiyo, huku Urusi ikitarajia kupenya ili kurejesha mpango huo baada ya kushindwa katika msimu wa kiangazi. Rais wa Urusi Vladimir Putin anatazamiwa kutoa hotuba muhimu siku ya Jumanne mjini Moscow, ambayo inatazamiwa kuhusika kwa kiasi kikubwa katika vita vya Ukraine.

Mkuu wa Ikulu ya Kremlin alianzisha uvamizi wa jirani yake mnamo Februari 24, 2022, akidai kwamba Kyiv ilikuwa akipanga mauaji ya halaiki ya watu wanaozungumza Kirusi huko Mashariki na kwamba nchi za Magharibi zilitaka kutumia ardhi ya Ukraine kudhoofisha Urusi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.