Pata taarifa kuu

Ukraine: Kiongozi wa Wagner adai kutekwa kwa Paraskoviïvka, karibu na Bakhmout

Yevgeny Prigojine, kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Urusi la Wagner, amesema siku ya Ijumaa Februari 17 kwamba wanajeshi wake wameuteka mji wa Paraskoviïvka nchini Ukraine, mji ulio kaskazini mwa Bakhmout na eneo la mapigano ya muda mrefu zaidi katika jimbo la Donbass tangu mwaka mmoja uliopita. 

Kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Urusi, Wagner,  Yevgueni Prigojine, Agosti 9, 2016, wakati wa mkutano wa kilele kati ya Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, mjini Saint Petersburg.
Kiongozi wa kundi la wanamgambo wa Urusi, Wagner, Yevgueni Prigojine, Agosti 9, 2016, wakati wa mkutano wa kilele kati ya Rais wa Urusi Vladimir Putin na mwenzake wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, mjini Saint Petersburg. AP - Alexander Zemlianichenko
Matangazo ya kibiashara

"Licha ya kushindwa kupata risasi na vifaa vingine vya jeshi, licha ya hasara kubwa na vita vya umwagaji damu, watu wetu wamefanikiwa kudhibiti eneo lote la Paraskoviïvka," Yevgeny Prigozhin amesema, akiinukuliwa na idara yake ya habari.

Kwa mali ya Warusi, EU inakwenda 'kwa hatua'

Kuundwa kwa Mahakama Maalum kwa ajili ya Ukraine, kutaifishwa kwa mali za Urusi zilizozuiwa: Umoja wa Ulaya siku ya Ijumaa ulitetea mkabala wa "hatua kwa hatua" kwa maombi haya mawili kutoka Kyiv ambayo yanazua maswali tata ya kisheria.

"Tunataka kuhakikisha kwamba wahalifu wote wa aina zote za uhalifu (uliotendwa nchini Ukraine) watafikishwa mahakamani, na kwamba Urusi italipa kwa ajili ya ujenzi na fidia" ya waathiriwa, amesema Kamishna wa Haki wa Ulaya Didier Reynders , wakati wa mkutano na waandishi wa habari na Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Ukraine, Andriï Kostin.

Paris na Berlin wanataka 'kuongeza' juhudi zao kwa ajili ya Ukraine

"Lazima tuzidishe msaada wetu na juhudi zetu za kusaidia upinzani wa watu wa Ukraine na jeshi na kuwawezesha kuongoza mapambano ambayo peke yake yatawezesha mazungumzo ya kuaminika chini ya masharti yaliyochaguliwa na Ukraine", ameomba rais wa Ufaransa Emmanuel Macron katika mkutano wa usalama wa Munich ulioanza siku ya Ijumaa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.