Mawaziri wa ulinzi kutoka Jumuiya ya NATO wakutana Brussels
NAIROBI – Mawaziri wa ulinzi kutoka jumuiya ya NATO pamoja na Marekani, wamekubaliana kuongeza kasi ya kuisaidia silaha zaidi nchi ya Ukraine, wakati huu Urusi ikizidisha mashambulio mashariki mwa nchi hiyo.
Imechapishwa:
Cheza - 00:36
Katika kikao chao cha Brussels, Ubelgiji, mawaziri hao wamesema Urusi itaendelea kufanya kosa kama inafikiria nchi hizo zitasitisha msaada wake kwa Ukraine, na kwamba hivi karibuni nchi zao zitatuma silaha zaidi.
Lloyd Austin, ni waziri wa ulinzi wa Marekani.
“Tulichukua hatau kwa haraka, haraka ambayo ilihitajika kwa wakati husika na mara zote imetutaka tuchukue hatua kwa vile tulivyoahidi kwa Ukraine. ”amesemaLloyd Austin, ni waziri wa ulinzi wa Marekani
Mkutano huu unakuja wakati huu Ukraine ikitoa wito kwa washirika wake kutuma silaha zaidi zikiwemo za masafa marefu na ndege za kivita ilikupiga jeki azma yake ya kujilinda kutokana uvamizi wa Urusi nchini wake.