Pata taarifa kuu
USALAMA-ULINZI

Ukraine yalengwa na mashambulio mapya ya makombora ya usiku

Ukraine imekumbwa na mashambulizi mapya ya makombora na mashambulizi mengie yaliyofanywa na ndege zisizo na rubani usiku, milipuko ambayo iliua takriban raia mmoja na kuharibu nyumba nyingi, kulingan ana mamlaka ya Ukraine.

Tangu mwezi Oktoba, Urusi imekuwa ikifanya kampeni ya mashambulizi makubwa ya mabomu dhidi ya miundombinu muhimu nchini Ukraine katika jaribio la kuwanyima wakazi, katikati ya majira ya baridi, umeme na joto.
Tangu mwezi Oktoba, Urusi imekuwa ikifanya kampeni ya mashambulizi makubwa ya mabomu dhidi ya miundombinu muhimu nchini Ukraine katika jaribio la kuwanyima wakazi, katikati ya majira ya baridi, umeme na joto. REUTERS - MARKO DJURICA
Matangazo ya kibiashara

 

Kwa mujibu wa Jeshi la Anga, makombora 16 kati ya 32 yaliyorushwa usiku na Urusi kutoka kwa ndege na meli katika Bahari Nyeusi yalidunguliwa.

"Kwa bahati mbaya, kulikuwa na athari kaskazini na magharibi, na pia katika mikoa ya Dnipropetrovsk na Kirovograd," mkuu wa utawala wa rais wa Ukraine Andriy Iermak amesema kwenye Telegram.

Angalau mtu mmoja auawa

Gavana wa mkoa wa Dnipropetrovsk, Serguiï Lyssak, amerusha picha za lori za kikosi cha Zimamoto zikifanya kazi katika mtaa ambapo nyumba za watu binafsi ziliharibiwa vibaya. Angalau mtu mmoja, mwanamke mwenye umri wa miaka 79, ameuawa.

Gavana wa mkoa wa Lviv (magharibi), Maxime Kozytsky, kwa upande wake amesema kuwa mashambulizi yamepiga "miundombinu muhimu" bila kusababisha hasara yoyote. Moto umedhibitiwa.

Tangu mwezi Oktoba, Urusi imekuwa ikifanya kampeni ya mashambulizi makubwa ya mabomu dhidi ya miundombinu muhimu nchini Ukraine katika jaribio la kuwanyima wakazi, katikati ya majira ya baridi, umeme na joto. Moscow pia inashukiwa kuandaa mashambulizi mapya makubwa mwishoni mwa majira ya baridi au masika, baada ya miezi kadhaa ya vikwazo vya kijeshi na mwaka mmoja baada ya kuanza kwa uvamizi wake nchini Ukraine.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.