Pata taarifa kuu
URUSI- UKRAINE- MAPIGANO

Ukraine imedai kuangusha maputo ya kijasusi ya Urusi

NAIROBI – Maafisa wa kijeshi nchini Ukraine wanasema, wameangusha maputo sita ya kijasusi kutoka Urusi, yaliyokuwa katika anga lake jijini Kyiv.

Ukraine imedai kuangusha maputo ya Urusi
Ukraine imedai kuangusha maputo ya Urusi REUTERS - GLEB GARANICH
Matangazo ya kibiashara

Katika hatua nyingine, Umoja wa Mataifa, umesema, kiasi cha dola za Marekani Bilioni 5.6 kinahitajika mwaka huu ili kutoa misaada ya kibinadamu nchini Ukraine.

Martin Griffiths, ni mkuu wa tume ya misaada ya kibinadamu ya umoja wa Mataifa.

“Tunalenga kuwafikia watu zaidi ya milioni kumi na moja kupitia mpango huu.” ameeleza Martin Griffiths.

Wito huu umekuja kuelekea mwaka mmoja tangu Urusi ilipoivamia nchi hiyo, itakapotimia tarehe 24 mwezi huu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.