Pata taarifa kuu

Rais Joe Biden yuko nchini Poland akitokea Ukraine

NAIROBI – Rais wa Marekani Joe Biden, yuko nchini Poland kwa ziara akitokea Ukraine ambako alifanya safari ya kushtukiza hapo jana, ambapo aliahidi nchi yake kutoa kiasi cha dola milioni 500 kununua silaha kwa ajili ya Kiev.

Rais wa Marekani Joe Biden anafanya ziara nchini Poland baada ya kufanya ziara nchini Ukraine ambapo amefanya kikao na rais Volodymyr Zelenskiy
Rais wa Marekani Joe Biden anafanya ziara nchini Poland baada ya kufanya ziara nchini Ukraine ambapo amefanya kikao na rais Volodymyr Zelenskiy via REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

“Mwaka mmoja baadae Kyiv bado imesimama na Ukraine imesimama, demokrasia imesimama na Marekani pia imesimama na wewe. ”amesema rais wa Marekani Joe Biden.

Ziara ya Biden nchini Ukraine, imekuja siku chache kabla ya maadhimisho ya mwaka mmoja tangu Urusi ivamie Ukraine, Februari 24 mwaka jana.

Mataifa mengine ya Magharibi yameendelea kutangaza kuisaidia nchi ya Ukraine dhidi ya uvamizi wa Urusi nchini mwake, Moscow kwa upande wake ikizituhumu nchi hizo kwa kuwa na njama ya kuiharibu Urusi kupitia kwa Ukraine madai ambayo mataifa hayo yamekanusha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.