Pata taarifa kuu

Ukraine: Watano wauawa katika mashambulizi ya angani Kherson

Takriban watu watano wameuawa Jumanne, Februari 21, katika shambulio la Urusi huko Kherson, mji ulioko kusini mwa Ukraine uliotekwa tena na jeshi la Ukraine mnamo Novemba 2022, ametangaza Vladislav Nazarov, afisa wa kijeshi wa mkoa huo, shirika la habari la AFP limeripoti.

soko  na vituo vya usafiri wa umma" "vililengwa kwa mashambulizi hayo", amesema msemaji wa kamandi ya jeshi la Ukraine, Vladislav Nazarov.
soko na vituo vya usafiri wa umma" "vililengwa kwa mashambulizi hayo", amesema msemaji wa kamandi ya jeshi la Ukraine, Vladislav Nazarov. REUTERS - LISI NIESNER
Matangazo ya kibiashara

Mji wa Kherson, kusini mwa Ukraine, uliotekwa tena na jeshi la Ukraine mnamo mwezi Novemba, ulikumbwa na mashambulizi ya angani sambamba na hotuba ya Vladimir Putin, Jumanne Februari 21, ametangaza kwenye Telegram msemaji wa kamandi ya jeshi la Ukraine, Vladislav Nazarov. 

"Wakati wa hotuba ya dikteta Vladimir Putin, adui alitekeleza mashambulizi dhidi ya majengo ya makazi, miundombinu muhimu," alisema. Aliongeza kuwa hospitali, "soko  na vituo vya usafiri wa umma" "vililengwa kwa mashambulizi hayo". 

Takriban raia watano waliuawa na 16 kujeruhiwa, kulingana na ripoti ya hivi punde. Ripoti ya awali iliripoti kuwa watu sita waliuawa na kumi na wawili kujeruhiwa, kabla ya kufanyiwa marekebisho baadaye na utawala wa manispaa ya Kherson.

  Kyiv inataka "kuwinda na kuadhibu" Urusi. "Kwa ufupi, [Warusi] wako kwenye mkanganyiko kimkakati. Kazi yetu ni kuwafukuza kutoka Ukraine na kuwaadhibu kwa kila kitu," amesema Andriy Yermak, mkurugezi katika ofisi ya Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky, kwenye ujumbe wa Telegram, baada ya hotuba ya kila mwaka ya Vladimir Putin kwa taifa la Urusi

Urusi inajiondoa kwa muda kutoka kwa Mkataba wa New Start

Wakati huo huo Vladimir Putin ametangaza kuwa Urusi inasitisha ushiriki wake katika mkataba wa kimkakati wa kupunguza silaha za nyuklia uliotiwa saini na Marekani. Wizara ya Ulinzi na Rosatom wanapaswa kujiandaa kufanya majaribio ya nyuklia ikiwa ni lazima, ameongeza, lakini ikiwa tu Marekani itafanya hivyo kwanza. Mnamo mwezi Januari, NATO iliomba Moscow kuruhusu wakaguzi katika mitambo ya slaha za kimkakati, kama inavyotakiwa na mkataba. Lakini Urusi ilikuwa tayari imetangaza mwanzoni mwa mwezi Agosti kusitisha ukaguzi huu wa Marekani, na kuhakikisha kwamba ilikuwa ikikabiliana na vikwazo vya Marekani kwa ukaguzi wa Urusi nchini Marekani. Katibu Mkuu wa NATO Jens Stoltenberg amesema 'anasikitisjhwa'na  uamuzi huo.

Mataifa ya Magharibi yanataka 'kuiangamiza' Urusi, kulingana na Vladimir Putin

 Rais wa Urusi ametoa hotuba yake ya kila mwaka kwa taifa siku ya Jumanne, karibu mwaka mmoja baada ya kuanzisha mashambulizi yake ya kijeshi nchini Ukraine. Ametoa hotuba yake mbele ya viongozi wa kisiasa wa nchi hiyo na wanajeshi wanaopigana nchini Ukraine. Vladimir Putin amehakikisha kwamba nchi yake "itafikia malengo [yake]". Haishangazi, kisha ameshtumu nchi za Magharibi, ambaye amelaani mwenendo wao na kushutumu kutumia mzozo wa Ukraine 'kuiangamiza' Urusi. "Wasomi wa Magharibi hawafichi lengo lao: kusababisha Urusi ishindwe kimkakati katika vita viavyoendelea," amebainisha.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.