Pata taarifa kuu
MAANDAMANO-HAKI

Maandamano makubwa ya kutetea mfumo wa afya ya umma yafanyika Madrid

Kwa mara ya tatu katika kipindi cha miezi mitatu, mamia ya maelfu ya waandamanaji wameandamana Jumapili hii, Februari 12 katika mitaa ya mji mkuu wa Uhispania kushutumu ukosefu wa wafanyakazi na uwezo katika mfumo wa afya ya umma.

Kwa mara ya tatu kipindi cha miezi mitatu, mamia ya maelfu ya waandamanaji wameandamana katika mitaa ya Madrid Jumapili Februari 12 kulaani ukosefu wa wafanyakazi na uwezo katika mfumo wa afya ya umma.
Kwa mara ya tatu kipindi cha miezi mitatu, mamia ya maelfu ya waandamanaji wameandamana katika mitaa ya Madrid Jumapili Februari 12 kulaani ukosefu wa wafanyakazi na uwezo katika mfumo wa afya ya umma. REUTERS - VIOLETA SANTOS MOURA
Matangazo ya kibiashara

Waandamanaji milioni moja ndio walioandamana katika mitaa ya Madrid, kulingana na vyama vya wafanyakazi. Manispaa ya jiji la Madrid, kwa upande wake, imetaja idadi ya watu 250,000 walioandamana, ishara kwamba uhamasishaji umeongezeka katika miezi na wiki za hivi karibuni kwa wakaazi wa Madrid.

Ingawa eneo hili ndilo tajiri zaidi nchini, liko katika nafasi ya mwisho kati ya mikoa 18 ya Uhispania katika suala la uwekezaji katika afya ya umma, kwa euro 1,491 kwa mwaka na kwa kila mkazi, kulingana na ripoti ya hivi karibuni kutoka Wizara ya Afya ya mwaka 2020.

Mgomo wa wahudumu wa afya

Imeshuhudiwa katika mji mkuu wa Uhispania mfululizo wa mgomo wa madaktari wa afya ya msingi ambao wanalalamikia ukosefu wa uwezio, wafanyakazi na pesa. Kama athari, karibu 80% ya wahudumu wa afya hutoroka nchi na hasira inaelekezwa dhidi ya Isabel Diaz Ayuso, rais wa serikali ya mkoa wa Madrid. “Madaktari sio tunachokosa. Shida ni kwamba wanalazimika kwenda kutafuta kazi sehemu nyingine, sijui wapi. Hapa mfumo haufanyi kazi. Kwa sababu hatuajiri madaktari wa kutosha, "anashutumu Josefa, mmoja wa wahudumu wa afya waliyostaafu.

Rais wa Madrid Isabel Diaz Ayuso amesema hataki kufanya mazungumzo. Lakini inawezekana kwamba atalazimika kufanya mazungumzo, kutokana na hali ambayo inatisha.

(Pamoja na AFP)

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.