Pata taarifa kuu

Uhispania: Idadi ya wahamiaji wanaowasili katika Visiwa vya Canary yaongezeka

Visiwa vya Canary nchini Uhispania, karibu na pwani ya Afrika, vimeshuhudia kuongezeka kwa idadi kubwa ya wahamiaji katika siku za hivi karibuni.

Boti kutoka Moroko kwenye pwani ya Gran Canarias, mnamo Oktoba 2020.
Boti kutoka Moroko kwenye pwani ya Gran Canarias, mnamo Oktoba 2020. © AP - Javier Bauluz
Matangazo ya kibiashara

 

Usiku wa Jumapili Agosti 14 hadi Jumatatu Agosti 15, meli iliyokuwa na wahamiaji 48 waliokolewa kwenye pwani ya ya kisiwa cha Fuerteventura. Wahamiaji watatu walikufa maji wakati walipokuwa wakijaribu kuokolewa... Kwa jumla, karibu wahamiaji 700 waliwasili siku nne zilizopita katika Visiwa vya Canary. Wengi wao wakiwa kwenye boti ndogo, zilizojaa kupita kiasi, ambazo zilivuka pwani ya Morocco.

Siku ya Ijumaa ya wiki iliyopita, watu 392 waliokolewa kweye pwani ya kisiwa cha Lanzarote, katika boti 8 ndogo. Shughuli za kuwasaidia zilikumbwa na sintofahammu na zilionekana kuwa ngumu. Mamlaka ililazimika kutumia helikopta mbili, pamoja na boti zinazosafiri katika eneo hilo ili kuweza kuwaokoa wahamiaji wote.

Jumamosi na Jumapili, watu wengine 323 waliokolewa. Kutokana na hali ya bahari kuwa ngumu, baadhi ya abiria haweza kuendelea na safari yao.

Vituo vya usaidizi viko chini ya shinikizo

Barabara hii inayoelekea Ulaya imeshuhudia ongezeko la idadi kubwa ya wahamiaji katika wiki za hivi karibuni kutokana, miongoni mwa mambo mengine, kuimarishwa kwa ukaguzi kwenye pwani ya Mediterania, hatua iliyochukuliwa na mamlaka ya Morocco.

Ongezeko hili kubwa la wahamiaji kutoka Kusini mwa Jangwa la Sahara na Maghreb limeweka shinikizo kwa vituo vya misaada katika Visiwa vya Canary na hasa huko Lanzarote.

 Katika nusu ya kwanza ya mwaka 2022, karibu watu 800 wamepoteza maisha katika barabara hii, kulingana na ripoti ya shirika lisilo la kiserikali laa Caminando Fronteras. Au kwa wastani: vifo vitano kwa siku kati ya mwezi wa Januari na Juni.

Na sio Visiwa vya Canary pekee vinavyokumbwa na hali hii, Visiwa vya Balearic pia vimeshuhudia idadi kubwa ya wahamiaji, zaidi ya 45% ya wahamiaji mwaka huu, kulingana na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Uhispania.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.