Pata taarifa kuu

Guinea: Wahamiaji 146 wanaorejea kwa hiari warejeshwa makwao na IOM kutoka Niger

Wahamiaji mia moja na arobaini na sita wa Guinea kutoka Niger waliweza kurejea nchini mwao Alhamisi Februari 10 kwa kutumia ndege iliyokodishwa na Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM).

IOM hupanga safari za ndege kuwarejesha makwao wahamiaji wanaorejea kwa hiari.
IOM hupanga safari za ndege kuwarejesha makwao wahamiaji wanaorejea kwa hiari. AFP PHOTO/BULENT KILIC
Matangazo ya kibiashara

Kwa ujumla, katika mwezi huu wa Februari, shirika la kimataifa la IOM linaandaa safari tatu maalum za ndege, kwa wahamiaji ambao wamejaribu kwenda Ulaya kupitia Bahari ya Mediterania, Wahamiaji hao wanarejea kwa hiari.

Wahamiaji hao 146 waliorudishwa hivi karibuni nchini Guinea, wana uwezekano wa kupata chanjo dhidi ya Covid.

"Katika kundi hili kuna hasa vijana, wanawake wachache, ambao walikuwa "njiani" kwa matumaini ya kufikia pwani za Ulaya. Safari ndefu na katika mazingira hatarishi.

Tukio jipya: wahamiaji hawa walipitia shule kuliko wale wa hapo awali, kama anavyobaini Lucas Chandellier, afisa mawasiliano wa IOM nchini Guinea.

Safari nyingine ya kuwarejesha makwao raia wa Guinea kutoka Niger imepangwa kufanyika Februari 17. Mwaka jana, Shirika la Kimataifa la Uhamiaji lilipanga kuwarejesha makwao wahamiaji 4,000 wa Guinea.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.