Pata taarifa kuu
MAREKANi

Suala la wahamiaji wa Haiti: Afisa mwandamizi wa Marekani ajiuzulu

Sintofahamu inaendelea kujitokeza kufuatia kufukuzwa kwa umati wa wahamiaji wa Haiti nchini Marekani na kuwarejesha katika nchi yao ya asili. Mooja wa maafisa waandamaizi nchini Marekani, Harold Koh, amejiuzulu.

Harold Koh, Mshauri wa masuala ya Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Juni 28, 2011 huko Washington.
Harold Koh, Mshauri wa masuala ya Sheria katika Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, Juni 28, 2011 huko Washington. Getty Images via AFP - CHIP SOMODEVILLA
Matangazo ya kibiashara

Baada ya kujiuzulu kwa mjumbe maalum kwa Haiti Daniel Foote, afisa mwingine mwandamizi wa Marekani ameamua kujiuzulu. Harold Koh, mwanasheria aliyebobea na mkuu wa zamani wa Chuo Kikuu cha Yale, alituma nakala yenye kurasa sita kwa wakuu wake akielezea uamuzi wake.

 

 

Katika nakala hii, ambayo gazeti la Politico lilipata kopi yake, Harold Koh ameelezea wazi kilicho sababisha anachukuwa uamuzi wa kujiuzulu. Umaskini uliokithiri, machafuko yanayosababishwa na magenge yenye silaha, kuongezeka kwa mivutano ya kisiasa baada ya mauaji ya rais Jovenel Moïse, tetemeko la ardhi, kimbunga cha kitropiki: "Haiti inakumbwa na jinamizi la kibinadamu". Kwa kuwarejesha wahamiaji wa Haiti katika nchi yao, utawala wa Biden unakiuka sheria za kimataifa, amesema afisa huyo mwandamizi katika Wizara ya mambo ya Nje ya Marekani.

Kulingana na takwimu za hivi punde kutoka Shirika la Kimataifa la Uhamiaji (IOM), ndege 57 kutoka Marekani zilitua ncini Haiti kati ya Septemba 19 na Oktoba 1, na kupeleka wahamiaji 6,213 nyumbani.

Mnamo Septemba 22, mjumbe maalum wa Haiti Daniel Foote alitangaza kujiuzulu kupitia barua aliyomuandikia Waziri wa mambo ya Nje wa Marekani Antony Blinken. Alilaani "uamuzi unaokiuka hakli za binadamu na usio na tija wa Marekani kwa kuwafukuza maelfu ya wakimbizi wa Haiti na wahamiaji haramu nchini Haiti".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.