Pata taarifa kuu
HISPANIA-MONKEYPOX

Monkeypox yaua watu wiwili nchini Hispania

Hispania imeripoti kifo cha pili cha mgonjwa wa monkeypox siku moja baada ya kutanagaza kifo cha kwanza kutokana na kile kilichoaamnika kuwa maambukizi ya monkeypox.

Chanjo ya maambukizi ya monkeypox
Chanjo ya maambukizi ya monkeypox REUTERS - DADO RUVIC
Matangazo ya kibiashara

Ripoti ya wizara ya afya nchini humo inasema kati ya wagonjwa 3,750, 120 wamelazwa,  wawili kati yao wakidhibitishwa kufariki.

Kwa mujibu wa kituo cha kushugulikia majanga katika wizara ya afya nchini humo, watu 4,298 wameambukizwa monkeypox. Hispania sasa ikiwa taifa ambalo limeathirika pakubwa na maambukizi hayo duniani.

Nchi ya Brazil nayo pia siku ya Ijuma iliripoti kifo cha kwanza ambacho kimehusishwa na maambukizi ya monkeypox.

Mamlaka nchini Brazili haijaekwa wazi iwapo vifo vya watatu hao vilisababishwa na  maambukizi ya monkeypox.

Shirika la afya duniani WHO limetangaza maambukizi hayo kama janga la kiafya la kidunia.

Bara Europa, limesajili idadi kubwa ya visa vya monkeypox tangu mapema mwezi Mei,ambayo ni asilimia 70  kwa mujibu katibu mkuu wa WHO Tedros Adhanom Ghebreyesus.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.