Pata taarifa kuu

Kampeni za kisiasa kutamatika kuelekea duru ya pili ya uchaguzi wa urais

Nchini Ufaransa leo ni siku ya mwisho ya kampeni kuelekea mzunguko wa pili wa uchaguzi wa urais siku ya Jumapili, kati ya rais Emmanuel Macron na mpinzani wake Marine Le Pen

Marine Le Pen mgombea urais kupitia chama cha Rassemblement national na Emmanuel Macron, watamenyana katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Ufaransa, Aprili 24, 2022.
Marine Le Pen mgombea urais kupitia chama cha Rassemblement national na Emmanuel Macron, watamenyana katika duru ya pili ya uchaguzi wa urais nchini Ufaransa, Aprili 24, 2022. AFP - PASCAL GUYOT
Matangazo ya kibiashara

Wawili hao wanamalizia kampeni zao leo, kila mmoja akionekana kuwa na matumaini ya kuibuka mshindi siku ya Jumapili.

Rais Macron, atamalizia kampeni zake katika mji wa  Figeac, Kusini Magharibi wa Ufaransa, êneo ambalo alipata kura nyingi katika uchaguzi wa mzunguko wa Kwanza wiki mbili zilizopita.

Bi. Lepen naye atakuwa anamalizia kampeni zake katika ngome yake ya Abbeville, Kaskazini mwa Ufaransa na jana akiendeleza kampeni zake katika mji wa Pas-de-Calais, na kuendelea kumshtumu mpinzani wake kama mtu asiyestahili kuchaguliwa.

Wawili hao walichuana vikali katika mdahalo wa Televisheni siky ya Jumatano, na kupata nafasi ya kueleza sera zao kwa mamilioni ya wapiga kura nchini Ufaransa.

Wachambuzi wa siasa na kura za maoni zinaonesha kuwa, kutakuwa na ushindai mkali, lakini Macron anatarajiwa kushinda kwa kupata  asilimia 55 ya kura.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.