Pata taarifa kuu

Ufaransa: Watu waandamana kupinga sera za Le Pen kuhusu uhamiaji

Maandamano makubwa yanafanyika nchini Ufaransa dhidi ya mgombea urais wa mrengo wa kulia Marine Le Pen, kuelekea duru ya pili ya uchaguzi Aprili 24, atakapopambana na rais Emmanuel Macron. 

Emmanuel Macron, na Marine Le Pen wanafanya kampeni kwa duru ya pili ya uchaguzi wa urais.
Emmanuel Macron, na Marine Le Pen wanafanya kampeni kwa duru ya pili ya uchaguzi wa urais. © AP/Jean-Francois Badias/Daniel Cole/Montage RFI
Matangazo ya kibiashara

Polisi nchini Ufaransa wanaonya kuwa maandamano hayo yaliyopangwa katika miji 30 nchini humo huenda ikashuhudia vurugu. 

Maandamano haya yanakuja wakati huu kampeni ikiingia katika wiki ya mwisho, huku waandamanaji wakipinga sera za Le Pen hasa kuhusu uhamiaji na kutoonekana kuunga mkono Ufaransa kuwa ndani ya Umoja wa Ulaya. 

Wiki hii, Le Pen ambaye kura za maoni zinaonesha kuwa anakaribiana mno na Macron aliahidi iwapo atashinda uchaguzi baadaye mwezi huu, ataitisha kura ya maoani kuhusu suala ya uhamiaji na lakini pia ataangalia upya ushirikiano wa Ufaransa katika jeshi la mataifa ya Magharibi NATO. 

Marine Le Pen, wakati akifanya kampeni katika eneo la Saint-Rémy-sur-Avre, amelaani maandamano hayo, anayosema sio ya kidemokrasia. 

Wakati hayo yakijiri, rais Macron ameendeleza kampeni zake leo, katika mji wa pili kwa ukubwa wa Marseille, ngome ambayo aliyekuwa mgombea Jean Luc Melanchon, alipata kura nyingi.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.