Kampeni za uchaguzi wa kuwania kiti cha urais katika duru ya pili zaendelea Ufaransa
Nchini Ufaransa, rais Emmanuel Macron na Marine Le Pen wanaendeleza kampeni ya kusaka kura za kushinda urais, kuelekea duru ya pili Aprili 24.
Imechapishwa:
Macron ambaye amepata uungwaji mkono wa rais wa zamani François Hollande, leo amezuru Kanisa la Notre Dame jijini Paris, wakati huu pia akitoa mtazamo wake kuhusu mshahara mkubwa wa Mkurugenzi wa kampuni ya kutengeneza magari, Stellantis.
Naye Marine Le Pen anaendeleza kampeni zake, Kusini mwa nchi hiyo na amesema iwapo ataingia madarakani ataitisha kura ya maoani kuhusu suala tata la wahamiaji.
Kura za maoni zinaonesha kuwa kutakuwa na ushindani mkali kati ya wawili hao lakini, Macron anatarajiwa kuibuka mshindi