Ufaransa: Wagombea urais warushiana cheche za maneno kuelekea duru ya pili ya uchaguzi
Nchini Ufaransa, wagombea wa urais, rais Emmanuel Macron na Marine Le Pen wameendelea na kampeni kuelekea duru ya pili ya uchaguzi wa urais Aprili 24.
Imechapishwa:
Wagombea hao wawili wamerushiana maneno makali baada ya maafisa wa usalama kumzuia, mwanamke aliyekuwa anaadamana kumshtumu Le Pen kwa kuwa karibu na rais wa Urusi Vladimir Putin baada ya kutoa sera yake ya kigeni iwapo atashinda uchaguzi.
Macron ambaye leo anaendelea na kampeni zake Magharibi mwa nchi, amemshtumu mpinzani wake kwa kuwa na mitizamo mikali aliyoiita ya kiimla.
Awali, Macron aliziita sera za Le Pen za ubaguzi wa rangi.
Naye, Le Pen amekataa kuomba radhi kuhusu misimamo yake hasa será ya mambo ya nje baada ya kukabiliwa na mwandamanaji.
Katika hatua nyingine, wagombea hao wawili wanajiandaa kumenyana katika mjadala wa televisheni wiki ijayo April 20 na kurushwa moja kwa moja kwenye Televisheni za TF1, France 2, Franceinfo miongoni mwa vyombo vingine vya Habari.