Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHAGUZI

Matokeo ya mwisho ya uchaguzi: Macron aibuka mshindi kwa 27.85% ya kura

Rais wa Ufaransa anayemaliza muda wake Emmanuel Macron aliibuka mshindi, Jumapili, Aprili 10, katika duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais kwa 27.85% ya kura, mbele ya Marine Le Pen (23.15%) ambaye atachuana naye katika duru ya pili, naye Jean-Luc Mélenchon alishindwa kuingia katika duru ya pili licha ya kupata 21.95% ya kura, kulingana na matokeo ya mwisho ya uchaguzi wa urais yaliyotolewa Wizara ya Mambo ya Ndani.

Matokeo ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Ufaransa 2022.
Matokeo ya duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais nchini Ufaransa 2022. © NERACOULIS Alexandre
Matangazo ya kibiashara

Kiwango cha watu waliojiandikisha ambao hawakupiga kura kilifikia kilifikia 26.31% , kiwango cha juu zaidi kwa duru ya kwanza ya uchaguzi wa urais baada ya kiwango cha 28.4% mwaka 2002.

Marine Le Pen (RN) alichukuwa nafasi ya kwanza katika wilaya 20,036, na Emmanuel Macron (LREM) katika manispaa 11,861, kati ya jumla ya manispaa 35,080.

Rais anayeondoka Emmanuel Macron na mgombea wa RN Marine Le Pen wamejipatia nafasi ya kuingia katika duru ya pili baada ya kupata kura zinazohitajika kuingiakatika duru ya pili itakayofayika mnamo Aprili 24.

Hakuna mshindi aliyefikisha kura zinazohitajika kwa kura rais katika duru ya kwanza ya uchaguzi, mshindi alitakiwa kupata asilimia 50 za kura zote zilizohesabiwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.