Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHAGUZI

Ufaransa inafanya uchaguzi wa urais

Raia wa Ufaransa wanapiga kura Jumapili hii Aprili 10, 2022, katika duru ya kwanza kumchagua rais, wakati huu wadadisi wa siasa nchini humo wakitabari kuwa, kutakuwa na ushindani kati ya rais Emmanuel Macron na mwanasiasa wa siasa za mrengo wa kulia Marine Le Pen.

Afisa akiwa amebeba sanduku la kura anapotayarisha kituo cha kupigia kura kwa ajili ya uchaguzi wa urais, huko Le Touquet-Paris-Plage, Ufaransa Aprili 6, 2022.
Afisa akiwa amebeba sanduku la kura anapotayarisha kituo cha kupigia kura kwa ajili ya uchaguzi wa urais, huko Le Touquet-Paris-Plage, Ufaransa Aprili 6, 2022. REUTERS - PASCAL ROSSIGNOL
Matangazo ya kibiashara

Vituo vya kupigia kura vimefunguliwa tangu saa mbili asubuhi saa za Paris, lakini raia wa Ufaransa wanaoishi nje ya nchi na wale wanaoshi katika visiwa vinavyomilikiwa na nchi hiyo, walipiga kura jana Jumamosi. 

Matokeo ya uchaguzi huo yanatarajiwa kufahamika leo Jumapili usiku, huku wadadisi wa siasa wakisema Macron atatofautiana na mpinzani wake Le Pen kwa asilimia kidogo na hivyo wawili hao watachuana katika duru ya pili Aprili 24. 

Ili kumpata mshindi katika duru ya kwanza, mgombea anapaswa kupata asilimia 50 ya kura zote. 

Mbali na Macron na Le Pen, kuna wagombea wengine 10 wanaosaka nafasi ya kuongoza taifa hilo la Ulaya, akiwemo mwanasiasa mkongwe mwenye siasa za mrengo wa kushoto Jean-Luc Melenchon, ambaye huenda akamaliza katika nafasi ya tatu. 

Kuna wasiwasi kuwa, huenda robo ya wapiga kura, wasijokeze kupiga kura hii leo. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.