Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHAGUZI

Ufaransa yajianda kwa uchaguzi wa urais Jumapili

Raia wa Ufaransa kesho wanapiga kura kumchagua rais wao mpya baada ya rais anayemaliza muda wake Emmanuel Macron kumaliza muluhula wake wa miaka mitano. Emmanuel Macron ni miongoni mwa wagombea urais 12 watakaosiriki katika kinyang’anyiro hiki, chenye upnzani mkubwa.

Picha za wagombea urais katika uchaguzi wa urais wa Ufaransa wa mwaka 2022 zinaonekana kwenye mabango karibu na makao makuu ya jiji la Appilly, Ufaransa, Aprili 6, 2022.
Picha za wagombea urais katika uchaguzi wa urais wa Ufaransa wa mwaka 2022 zinaonekana kwenye mabango karibu na makao makuu ya jiji la Appilly, Ufaransa, Aprili 6, 2022. REUTERS - BENOIT TESSIER
Matangazo ya kibiashara

Kura za maoni zinaendelea kuonesha kuwa kinyang’anyiro ni kati ya rais Emmanue Macron na Marine Le Pen. 

 Wagombea 12 wanatafuta nafasi ya kuingia Ikulu ya Elysée na sasa hatima yao ipo mikononi mwa wapiga kura, hasa kuwavutia wale ambao hawajafanya maamuzi. 

Uchaguzi wa Jumapili utafanyika katika kipindi ambacho Ufaransa kama mataifa mengine duniani, inapata madhara ya vita vya Ukraine na Urusi, ambavyo vimesabisha kupanda kwa gharama ya maisha pamoja na bei ya mafuta. 

Nchini Ufaransa, tafiti za hibi karibuni zilionesha kwamba raia nchini humo wana uhakika kwamba Rais wa sasa Emmanuel Macron ana nafasi kubwa ya kuibuka mshindi katika mzunguko wa kwanza wakati uchaguzi huo utakapofanyika Aprili 10.

Kwa mujibu wa kura ya maoni ya kampuni ya BVA iliyotolewa Ijumaa wiki iliyopita, asilimia 75 ya raia waliosajiliwa nchini humo, wana nia ya kupiga kura, japo wakati huu asilimia hiyo itashuka ikilinganishwa na mwaka 2017. 

Mgombea Urais Marine Le Pen ameonekana kama atakayefika kwenye duru ya pili ya Uchaguzi na Macron, ambapo watakutaka kwenye duru hiyo jinsi walivyofanya mwaka 2017, japo pia mgombea  Jean-Luc Melenchon ameongeza umaarufu wake katika siku za hivi maajuzi. 

Kura ya maoni ya hivi punde iliyochapishwa na Ifop-Fiducial siku ya Jumatatu, ilionyesha Macron akiongoza kwa asilimia 28 huku Le Pen akimfuata nyuma na asilimia 21 katika duru ya kwanza ya uchaguzi. 

Tahariri katika gazeti la kila siku la Ufaransa la Le Monde, ilitoa mfano wa kura ya maoni ya Ipsos-Sopra Steria iliyoidhinisha kwamba ilitabiri kujitokeza kwa asilimia 67 katika awamu ya kwanza, siku ya Jumatatu ikionya kuhusu hatari iliyopo, wakati huu kuna ongezeko la mfumuko wa bei, mabadiliko ya hali ya hewa, na vita vinavyoendelea nchini Ukraine. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.