Pata taarifa kuu
UFARANSA-UCHAGUZI

Ufaransa: Wagombea urais wanahitimisha kampeni zao kuelekea uchaguzi

Nchini Ufaransa, kuelekea uchaguzi wa rais siku ya Jumapili, mgombea Jean-Luc Mélenchon, anafanya mkutano wake wa mwisho hivi leo mjini Lille. 

Jean-Luc Mélenchon, mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha  La France Insoumise, wakati wa mkutano wake huko Place du Capitole, huko Toulouse, Jumapili Aprili 3.
Jean-Luc Mélenchon, mgombea wa urais kupitia tiketi ya chama cha La France Insoumise, wakati wa mkutano wake huko Place du Capitole, huko Toulouse, Jumapili Aprili 3. © AFP - LIONEL BONAVENTURE
Matangazo ya kibiashara

Mélenchon amekuwa katika miji mingine 11 akiomba kura, kuelekea uchaguzi huo ambao kura za maoni zinaonesha, wagombea wakuu ni rais Emmanuel Macron na Marine Le Pen. 

Kura za maoni zimekuwa zikimwonesha Mélenchon atamaliza katika nafasi ya tatu katika uchaguzi wa Jumapili na leo kwenye eneo la Grand Palais mjini Lille anatarajiwa kuwarai wapiga kura kumchagua. 

Kura za maoni hapo jana zilionesha kuwa alikuwa na asilimia 15.5 baada ya umaarufu wake kuongezeka kwa asililia 1.5 kwa kipindi cha wiki moja iliyopita. 

Hata hivyo, mpaka sasa kinyanyang'aniro kinaonekana kuwa kati ya rais Macron ambaye umaarufu wake umekuwa ukishuka licha ya kuongoza kwa asilimia 27.5, huku Le Pen akimkaribia kwa asilimia 22. 

Aidha, kura za maoni zinaonesha kuwa iwapo hakutakuwa na mshindi katia duru ya kwanza siku ya Jumapili, basi Macron ataibuka na ushindi katika duru ya pili kwa sasilimia 53 akifutwa na Le Pen kwa asilimia 47, Aprili 24. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.