Pata taarifa kuu

Uchaguzi Ufaransa: Vyama ya mrengo wa kushoto vyaanza mchakato wa kumchagua mgombea wao

Nchini Ufaransa, wafuasi wa siasa za mrengo wa kushoto wameanza kupiga kura ya maoni kwa njia ya mtandao, kumchagua mgombe urais mwenye umaarufu mkubwa, kuelekea Uchaguzi mwezi Aprili.

Vyama ya mrengo wa kushoto vyaanza zoezi la kumchagua mgombea wao kuelelea uchaguzi wa urais nchini Ufaransa.
Vyama ya mrengo wa kushoto vyaanza zoezi la kumchagua mgombea wao kuelelea uchaguzi wa urais nchini Ufaransa. REUTERS/Charles Platiau
Matangazo ya kibiashara

Watu zaidi ya 467,000 wanashiriki katika zoezi hilo, ambalo litaendelea hadi Jumapili wakati mshindi atakapotangazwa.

Wachambuzi wa siasa nchini humo wanaona kuwa, aliyewahi kuwa Waziri wa Sheria na Katiba, Christine Taubira anatarajiwa kuibuka mshindi.

Baadhi ya wagombea kama Jean-Luc Melenchon, Yannick Jadot kutoka mrengo wa kijani na aliyekuwa Meya wa jiji na Anne Hidalgo wanatarajiwa kupuuza matokeo ya kura hiyo ya maoni.

Kuelekea Uchaguzi wa mwezi Aprili, Rais Emmanuel Macron anapewa nafasi kubwa ya kuibuka mshindi, lakini wachambuzi wanasema chochote kinaweza kutokea kwa sababu ushindani unatarajiwa kuwa mkubwa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.