Pata taarifa kuu

Emmanuel Macron akumbana na upinzani wa wabunge wa Ulaya kutoka Ufaransa

Emmanuel Macron alikuwa, Jumatano hii, Januari 19, mbele ya Bunge la Strasbourg kutangaza vipaumbele vya urais wa Ufaransa wa Baraza la Umoja wa Ulaya na kutoa maono yake ya Ulaya, kabla ya kushiriki katika mjadala na wabunge.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron mbele ya Bunge la Ulaya huko Strasbourg, Januari 19, 2022.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron mbele ya Bunge la Ulaya huko Strasbourg, Januari 19, 2022. AP - Jean-Francois Badias
Matangazo ya kibiashara

Kama ilivyotarajiwa, kampeni ya uchaguzi wa urais nchini Ufaransa imeingizwa katika Bunge la Ulaya baada ya Emmanuel Macron Jumatano hii kulihutubia Bunge hilo. Mjadala uliofuata hotuba ya Rais wa Ufaransa Emmanuel Mcron katika jengo la bunge hilo huko Strasbourg kuashiria kuanza kwa uenyekiti wa Ufaransa wa Baraza la Umoja wa Ulaya haraka uligeuka kuwa mashindano na wabunge wa Ulaya kutoka Ufaransa walioshiriki kikao hicho, ambao walimshambulia rais wa Ufaransa.

Mbunge Yannick Jadot ameanza kwa maneneo ambayo wengi waliona kama ni chokochoko dhidi ya rais, kulingana na mwandishi wetu maalum huko Strasbourg, Anthony Lattier. "Utaingia katika historia, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri, kama rais ambaye hakutetea suala lonalohusiana na tabia nchi. Kwa sababu ndani kabisa, wewe ni mtetezi wa tabia nchi. Unapendelea kutia saini kwenye mikataba ya silaha badala ya kupigana vita dhidi ya mabadiliko ya tabia nchi," ameshutumu mgombea urais atakaye peperusha bendera ya chama cha Kijani katika uchaguzi wa urais nchini Ufaransa uliopangwa kufanyika mwezi Aprili mwaka huu.

Baada ya kuzomewa, na kushutumiwa kwa kufanya kampeni ya uchaguzi, Yannick Jadot alipokea wito kutoka kwa wabunge kadhaa wa Ulaya, ikiwa ni pamoja na Stéphane Séjourné, anaymuunga mkono Emmanuel Macron, wa kutaka aachane na kampeni hiyo, : "Ni aibu iliyoje kulifanya Bunge hili la Ulaya kuwa Bunge la kitaifa. »

Umuhimu wa maelewano

Lakini haijalishi, wapinzani wa Ufaransa wanaona "kuchukua" muda huu kuongelea kwa yale yanayowaaudhi katika Bunge la Ulaya, wakibaini kwamba Emmanuel Macron, kwa kutoomba kuahirishwa kwa urais wa Ufaransa wa Umoja wa Ulaya, alikuwa akijiweka wazi nia ya kuiingiza siasa katikati ya kampeni katika bunge hilo.

Rais wa Ufaransa amejibu hoja kwa hoja na akakumbusha haja ya kufanya maafikiano ili kuisogeza Ulaya mbele. "Ninashangaa kwamba mtu yeyote analaumiwa kwa kutia saini nakala kuhusu masuala ya kijamii, mazingira na nishati na nchi kama Poland na Hungary. Hivi ndivyo Ulaya yetu inavyofanya kazi. Vinginevyo, unazuia Ulaya kila wakati. »

Muda mfupi kabla, Emmanuel Macron alikuwa ameonya, katika hotuba yake, dhidi ya mashambulizi dhidi ya utawala wa sheria na alisisitiza haja ya "kila mahali kuwashinikiza tena watu waliojitenga". Ujumuishaji wa haki ya kutoa mimba na ulinzi wa mazingira katika Mkataba wa Haki za Msingi za Umoja wa Ulaya, lakini pia "amri mpya ya usalama" na NATO dhidi ya Urusi, mageuzi ya eneo la Schengen, "mapinduzi ya dijiti": rais wa Ufaransa ameweka vipaumbele vyake kwa Ulaya ikiwa na "njia za kujiamulia mustakabali wake".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.