Pata taarifa kuu

Ufaransa kuongoza EU: Emmanuel Macron ataka "Ulaya yenye nguvu na uhuru"

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron, ametaka Umoja wa Ulaya imara na huru, wakati huu nchi hiyo inapotarajiwa kuchukua hatamu za uongozi wa Umoja huo kuanzia Jánuari 1 mwaka 2022.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wakati wa mkutano na waandishi wa habari juu ya Ufaransa kuchukua uenyekiti wa EU, huko Paris, Desemba 9, 2021.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron wakati wa mkutano na waandishi wa habari juu ya Ufaransa kuchukua uenyekiti wa EU, huko Paris, Desemba 9, 2021. REUTERS - POOL
Matangazo ya kibiashara

Macron amekuwa akieleza baadhi ya mipango ya nchi yake, itakapoongoza Umoja huo wa nchi 27 unaoshirikiana katika masuala ya siasa na uchumi.

 

Hayo yanajiri wakati rais wa Ufaransa aliandaa Alhamisi hii mchana, Desemba 9, mkutano wa pili na waandishi wa habari kwa minajili ya kuwasilisha vipaumbele vya Ufaransa itakapokuwa mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya (PFUE). Ufaranza itakabidhiwa uenyekiti Januari 1, 2022 kwa kipindi cha miezi sita. Uongozi huo utaambatana na kampeni ya urais nchini Ufaransa mwezi Aprili na uchaguzi wa wabunge mwezi Juni.

Akiwa amesimama nyuma ya meza mbele ya waandishi wa habari zaid ya mia moja katika ukumbi wa sherehe, rais wa Ufaransa alitaka kuonyesha mipango ya Ufaransa itakapokuwa mwenyekiti wa Umoja wa Ulaya. Kwa muda mrefu ametetea umuhimu mkubwa wa kuimarisha uhuru wa Ulaya katika kuunga mkono uhuru wa kitaifa.

"Ikiwa tungehitimisha kwa sentensi moja lengo la uenyekiti huu, ningesema kwamba lazima tuhame kutoka Ulaya ya ushirikiano ndani ya mipaka yetu hadi Ulaya ambayo ina nguvu duniani, huru kabisa, inayojitegemea kwa maamuzi yake, "alisema Emmanuel Macron.

Kwa hivyo rais wa Ufaransa aliomba kuwepo na "uhuru wa kimkakati wa Ulaya": "Dhana hii ambayo ilionekana kutofikirika miaka minne iliyopita inafanya iwezekane kusisitiza kwamba sisi raia wa Ulaya, tuwe wanachama wa NATO au la [...], tuna vitisho vya pamoja na malengo ya pamoja. "

Kutafakari mfumo wa bajeti

Emmanuel Macron pia alipendekeza "kutafakari upya mfumo wa bajeti" wa Ulaya hadi sasa unaofafanuliwa na vigezo vya Maastricht. Pamoja na mzozo wa kiafya, "tunasimamisha matumizi ya sheria zetu za bajeti," alikiri rais wa Ufaransa. Itabidi turudi kwenye sheria ambazo pekee zinaruhusu muunganiko wa uchumi wetu. Swali sio tena la kuunga mkono au kupinga dhidi ya 3%. swali hilo limepitwa na wakati. Dokezo la sheria inayozuia nchi wanachama wa eneo la euro kuzidi kiwango cha nakisi ya bajeti ya 3%, iliyolegezwa wakati wa mgogoro wa kiafya.

"Tunataka Ulaya ambayo itaunda nafasi za kazi". Ikiwa ni "Ulaya ya ukosefu wa ajira", itakuwa "Ulaya ya vita", alionya rais, akitoa mfano wa Ulaya "iliyotengana" ya miaka ya 1930 ambayo ilichagua "mtengamano".

Ufaransa inatarajiwa kuchukua uongozi wa Umoja huo, utakaodumu kwa miezi sita, wakati huu barra hilo likikabiliwa na wimbi la wahamiaji wengi wanaoingia katika mataifa hayo wakitokea nchini Belarus.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.