Pata taarifa kuu
UFARANSA-USHIRIKIANO

Saudi Arabia: Macron atangaza mpango wa pamoja kwa Lebanon

Rais Emmanuel Macron amerejea Paris, mji mkuu wa Ufaransa baada ya mkutano wake na Mwanafalme wa Saudi Arabia, Mohammed ben Salman, ambaye amemtaka Waziri Mkuu wa Lebanon Najib Mikati ili kujaribu kutafuta suluhu la ugomvi wa kidiplomasia kati ya Beirut na Riyadh. Rais wa Ufaransa pia anasema aligusia suala la haki za binadamu.

Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman akutana na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron mjini Jeddah, Saudi Arabia, Jumamosi, Desemba 4, 2021. Juu, picha ya Mfalme Salman.
Mwanamfalme wa Saudia Mohammed bin Salman akutana na rais wa Ufaransa Emmanuel Macron mjini Jeddah, Saudi Arabia, Jumamosi, Desemba 4, 2021. Juu, picha ya Mfalme Salman. AP - Bandar Aljaloud
Matangazo ya kibiashara

Haki za binadamu lilikuwa moja ya masuala nyeti zaidi katika ziara hii nchini Saudi Arabia. Naye Emmanuel Macron ametaka kuhakikishia suala hili, baada ya mkutano wake na Mwanamfalme wa Saudi Arabia Mohammed ben Salman.

"Yalikuwa mazungumzo ya moja kwa moja, natumai yatafaa, na kama unavyojua mimi huwa na mbinu sawa ambayo ni kujaribu kuhifadhi mkondo huu na viongozi ili kupata matokeo yanayoonekana," amebaini rais wa Ufaransa. Njia ambayo italazimika kuthibitisha ufanisi wake kwa wakati.

Ziara hii pia imemwezesha Emmanuel Macron kujadili masuala ya kikanda kama vile nishati ya nyuklia ya Iran, na hasa hali ya Lebanon. rais macron ameelezea kuridhika kwake kwa kupata ahadi kutoka kwa Mohammed bin Salman za kufanya kazi na Ufaransa katika kuunga mkono raia wa Lebanon.

Kuhusu Lebanon, tulifanya kazi pamoja na kisha kwa pamoja tukamwita Waziri Mkuu Mikati muda mfupi uliopita ili kutuma ujumbe ulio wazi: Saudi Arabia na Ufaransa wanataka kujihusisha kikamilifu, ilikuwa wazi sana katika masharti aliyotumia. Tunataka kuhusika ili kuwaunga mkono raia wa Lebanon.

Emmanuel Macron anaamini kuwa ametimiza malengo yake wakati wa ziara hii katika eneo la Ghuba. Kurejea Paris kutamrudisha kwenye kampeni ambapo chama cha Republican kimemteua Valérie Pécresse kuwa mgombea urais.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.