Pata taarifa kuu
UFARANSA-USHIRIKIANO

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aanza ziara katika nchi tatu za Ghuba

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amewasili Ijumaa hii, Desemba 3, huko Dubai (Falme za Kiarabu), kituo cha kwanza katika ziara ya kikanda ambayo pia itampeleka hadi Doha (Qatar) na Jeddah (Saudi Arabia) siku ya Jumamosi.

Mwaka 2017, rais wa Ufaransa akizuru Abu Dhabi (picha ya kumbukumbu.
Mwaka 2017, rais wa Ufaransa akizuru Abu Dhabi (picha ya kumbukumbu. AFP - LUDOVIC MARIN
Matangazo ya kibiashara

Ziara ambayo lengo lake ni kuimarisha ushirikiano na nchi hizi za Ghuba wakati muhula wake wa miaka mitano unamalizika na kampeni ya urais wa Ufaransa inapamba moto.

Eric Zemmour ametangaza kuwania kiti cha urais katika uchaguzi wa urais, wakati wafuasi wa kundi la Les Républicains wanapiga kura kumteua mgombea wao na Emmanuel Macron anaelekea nchi za Ghuba.

Moja ya ziara za mwisho za muhula

Ziara hii ndogo ya kikanda kwa Falme za Kiarabu, Qatar na Saudi Arabia, ambayo itakuwa moja ya safari za mwisho za muhula wake, itamwezesha Emmanuel Macron kukutana na viongozi "ambao ni muhimu" na ambao, kulingana na Elysée, Ufaransa " lazima ifanye kazi" katika eneo la kimkakati.

Emmanuel Macron ana vipaumbele vitatu: kuimarisha mapambano dhidi ya ugaidi wa Kiislamu, usalama wa kikanda na kukuza mvuto wa Ufaransa. Uwekezaji umetangazwa na mikataba ilitiwa saini mnamo Desemba 3, hasa uuzaji wa ndge za kivita ziitwazo Rafale.

Ufaransa, mshirika mkubwa

Emmanuel Macron anakwenda Ghuba kwa nia ya kuonyesha kwamba Ufaransa ni mshirika muhimu. Hii pia ni njia ya kuonyesha, machoni pa Wafaransa, hadhi yake kama kiongozi anayehesabiwa kimataifa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.