Pata taarifa kuu
KENYA - BIASHARA

Ufaransa kusaidia Kenya kujenga shule ya Uhandisi

Serikali ya Ufaransa itatoa mkopo wa Euro Milioni 30 kutoka mfuko wake wa maendeleo FDA, kwa serikali ya Kenya kwa lengo la kujenga  chuo cha Uhandisi katika Chuo Kikuu cha Nairobi. 

Waziri wa Ufaransa wa  biashara za kigeni, Franck Riester
Waziri wa Ufaransa wa biashara za kigeni, Franck Riester © FMM-RFI
Matangazo ya kibiashara

Hatua hii imekuja baada ya ziara ya waziri anayehusika na biashara za kigeni na uwekezaji wa Ufaransa wakati wa ziara yake nchini Kenya Franck Riester wiki iliyopita. 

Mbali na hilo, waziri huyo akiambatana na wafanyibiashara kutoka nchini Ufaransa,  amesifia uhusiano wa kufanya biashara kati ya nchi hizo mbili lakini pia ukanda wa Afrika Mashariki  na ushirikiano katika sekta kama miundo mbinu, unaimarika. 

Kwa Zanzibar ni ishara nzuri sana kwa ushirikiano wa ufaransa na air France, kuwezekeza katika safari za ndege na kuunganisha kanda zetu, Afrika mashariki na Ufaransa lakini kipia, Zanzibara na Tanzania na Ufaransa.

 

Ziara yake pia ilimpeleka Rwanda na Uganda, kujadiliana kuhusu masuala ya biashara kati ya Ufaransa na mataifa hayo. 

waziri wa biashara za Kigeni nchini Ufaransa, akihojiwa na mwanahabari RFI Kiswahili , Victor Abuso
waziri wa biashara za Kigeni nchini Ufaransa, akihojiwa na mwanahabari RFI Kiswahili , Victor Abuso © FMM-RFI

Aidha, ziara yake ilimpeleka nchini Tanzania ambako alizindua safari za ndege la Shirika la AIR France kutoka Paris kwenda Zanzibar. 

Safari hizi zimerejea baada ya kuanza tangu mwaka 1974, na safari hizo sasa zitafanyika mara mbili kwa wiki, siku ya Jumanne na Jumamosi; 

Waziri Riester anaeleza umuhimu wa hatua hii. 

 

Tumejitolea kama serikali kuhakikisha kuwa uhusiano wetu unakuwa imara ndio sababu nilikuja kujionea namna miradi yetu inavyokwenda hasa hapa nchini Kenya, na pili kampuni zetu zimejitolea kuhakikisha kuwa tunaongeeza biashara kati yetu.

 

Rais Emmanuel Macron mwaka 2017, katika ziara yake barani Afrika akiwa nchini Burkina Faso, akizungumza na vijana alionesha nia yake ya kuimarshga uhusiano ya Ufaransa na Afrika, hasa kwa mataifa yanasiyozungumza lugha ya Kiingereza. 

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.