Pata taarifa kuu
BENIN-USHIRIKIANO

Ufaransa yakamilisha kurejesha vifaa vya Kifalme vya Benin

Hati ya uhamisho wa umiliki wa vifaa 26 ambavyo vitarejeshwa na Ufaransa kwa Benin imetiwa saini Jumanne, Novemba 9 katika Ikulu ya Elysee mbele ya Marais Emmanuel Macron na Patrice Talon, kuhitimisha mchakato ulioanzishwa miaka minne iliyopita.

Vifaa kutoka ufalme wa Dahomey, kwenye Jumba la Makumbusho la Quai Branly, huko Paris, Novemba 23, 2018
Vifaa kutoka ufalme wa Dahomey, kwenye Jumba la Makumbusho la Quai Branly, huko Paris, Novemba 23, 2018 © AFP - CHRISTOPHE ARCHAMBAULT
Matangazo ya kibiashara

Mara hati hiyo ikitiliwa saini, ndege ya mizigo inaondoka kuelekea Cotonou ambako vifaa hivyo vinasubiriwa Jumatano, Novemba 10, ikiwa ni pamoja na sanamu tatu kubwa za kifalme Bocio, viti vya enzi, viti na madhabahu vinazobebeka.

Mnamo Novemba 2017, huko Ouagadougou, rais wa Ufaransa Emmanuel Macron aliahidi kurejesha kwa muda au kikamilifu urithi wa Kiafrika ndani ya miaka mitano.

Miezi saba baadaye, mnamo Novemba 23, 2018, Élysée ilitangaza kurejeshwa kwa vifaa 26 nchini Benin: vitarejeshwa hasa, vifaa kutoka kwa ufalme wa zamani wa Danhomè, vilivyoporwa na Kanali Dodds mwaka 1892. Tangazo hilo lilitolewa siku ambayo wasomi Bénédicte Savoy na Felwine Sarr waliwasilisha ripoti ambayo Emmanuel Macron aliwaagiza kuhusu suala hili.

Kwa mujibu wa Felwine Sarr, tangazo hilo ni kitendo cha uwanzilishi: "Kwa kweli huu ni wakati wa kihistoria, kwa sababu historia inaanza kusonga mbele sasa. Na kile kilicho hatarini ni cha msingi kabisa, kwa hivyo ni ishara lakini kitakuwa na athari katika nyanja zingine za uhusiano. "

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.