Pata taarifa kuu
UFARANSA-USHIRIKIANO

UEA na Ufaransa zatia saini mkataba wa ununuzi wa ndege 80 aina ya 'Rafale'

Umoja wa Falme za Kiarabu umetia saini mkwenye mkataba wa unuzi wa ndege 80 za kivita aina ya "Rafale", zilizotengenezwa na kampuni ya Ufaransa ya Dassault Aviation, wakati wa ziara ya rais wa Ufaransa Emmanuel Macron huko Dubai, Ikulu ya Elysée imesebaini katika taarifa.

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Mwanamfalme Mohamed bin Zayed, wakati wa kutangazwa kwa mkataba wa ununuzi wa ndege 80 aina ya Rafale, Desemba 3, 2021 huko Dubai.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron na Mwanamfalme Mohamed bin Zayed, wakati wa kutangazwa kwa mkataba wa ununuzi wa ndege 80 aina ya Rafale, Desemba 3, 2021 huko Dubai. Thomas Samson AFP
Matangazo ya kibiashara

Mbali na ndege hizi aina ya "Rafale", Umoja wa Falme za Kiarabu pia umesaini makubaliano ya ununuzi wa helikopta kumi na mbili aina ya "Caracal". "Haya ni mafanikio makubwa ya ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi hizo mbili", imekaribisha Ikulu ya Elysée katika taarifa, ambayo shirika la habari la AFP limepata kopi.

 

Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amewasili Ijumaa hii, Desemba 3, huko Dubai (Falme za Kiarabu), kituo cha kwanza katika ziara ya kikanda ambayo pia itampeleka hadi Doha (Qatar) na Jeddah (Saudi Arabia) siku ya Jumamosi.

Ziara hii ndogo ya kikanda kwa Falme za Kiarabu, Qatar na Saudi Arabia, ambayo itakuwa moja ya safari za mwisho za muhula wake, itamwezesha Emmanuel Macron kukutana na viongozi "ambao ni muhimu" na ambao, kulingana na Elysée, Ufaransa " lazima ifanye kazi" katika eneo la kimkakati.

Emmanuel Macron ana vipaumbele vitatu: kuimarisha mapambano dhidi ya ugaidi wa Kiislamu, usalama wa kikanda na kukuza mvuto wa Ufaransa. Uwekezaji umetangazwa na mikataba ilitiwa saini mnamo Desemba 3, hasa uuzaji wa ndge za kivita ziitwazo Rafale.

Emmanuel Macron anakwenda Ghuba kwa nia ya kuonyesha kwamba Ufaransa ni mshirika muhimu. Hii pia ni njia ya kuonyesha, machoni pa Wafaransa, hadhi yake kama kiongozi anayehesabiwa kimataifa;

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.