Pata taarifa kuu
UFARANSA-USHIRIKIANO

Ufaransa na Qatar zawahamisha zaidi ya raia 300 wa Ufaransa na Afghanistan

Miezi mitatu na nusu baada ya kundi la Taliban kuchukuwa udhibiti wa mamlaka mjini Kabul, Ufaransa inaendelea na shughuli zake za kuwahamisha raia. Ndege iliyokodishwa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa imewahamisha zaidi ya watu 300 kutoka Afghanistan kuelekea Qatar.

Ndege ya shirika la ndege la Qatar Airways ikipaa na wageni kutoka uwanja wa ndege wa Kabul, Afghanistan siku ya Alhamisi, Septemba 9, 2021 (picha ya kumbukumbu).
Ndege ya shirika la ndege la Qatar Airways ikipaa na wageni kutoka uwanja wa ndege wa Kabul, Afghanistan siku ya Alhamisi, Septemba 9, 2021 (picha ya kumbukumbu). AP - Bernat Armangue
Matangazo ya kibiashara

Wizara ya Mambo ya Nje ya Ufaransa, Quai d'Orsay, imebaini kwamba imewahamisha Waafghan 258 wanaume kwa wanawake wanaotishiwa hasa, wakiwemo waandishi wa habari, lakini pia wasaidizi wa zamani wa jeshi la Ufaransa ambao hadi sasa walikuwa bado hawajaweza kuondoka nchini Afghanistan. Walihamishwa kutoka Kabul hadi Doha na watapelekwa Ufaransa mwishoni mwa wiki ijayo.

Kwenye ndege hii, pia kulikuwa na Wafaransa 11na takriban raia sitini wa Uholanzi, kulingana na takwimu rasmi.

Kwa mara nyingine tena, Qatar ilichukua nafasi kubwa katika operesheni hii. Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron amekaribisha Jumamosi hii msaada wa Qatar kuandaa zoezi hili la kuwahamisha Waafghan 258, "waliotishwa kwa sababu ya msimamo wao" au "mahusiano yao na Ufaransa", ambao watasafirishwa hadi nchini Ufaransa baada ya kupitia Doha.

"Naishukuru Qatar kwa jukumu lake tangu kuanza kwa mzozo na ambayo imewezesha kuandaa zoezi kadhaa," Emmanuel Macron, ambaye alikutana na Emir Sheikh Tamim bin Hamad Al Thani Ijumaa jioni  katika ziara yake ya Ghuba.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.