Pata taarifa kuu
UFARANSA

Emmanuel Macron: "Udharura ni kuhakikisha usalama wa raia wetu Afghanistan

Baada ya Taliban kuchukuwa madaraka nchini Afghanistan, na wakati maelfu ya raia wa Afghanistan wanajaribu kukimbia nchi hiyo, rais wa Ufaransa aamelihutubia taifa Jumatatu hii Agosti 16.

Rais Emmanuel Macron wakati wa hotuba yake kwa taifa, Agosti 16, 2021.
Rais Emmanuel Macron wakati wa hotuba yake kwa taifa, Agosti 16, 2021. © TFI / Screenshot de la diffusion internet
Matangazo ya kibiashara

Katika hotuba yake kupitia televisheni, Emmanuel Macron amesema kuwa raia wa Ufaransa na Waafghanistan waliosaidia Ufaransa usalama wao utalindwa. Hata hivyo, ndege mbili za vikosi maalum zitapelekwa Afghanistan, ameongeza rais wa Ufaransa.

Machafuko yanatawala huko Kabul, mji mkuu wa Afghanistan, nchi ambayo Taliban wamerudi kuchukuwa hatamu ya uongozi. Wanajeshi wa Marekani wameondoka - wanadhibiti tu uwanja wa ndege wa Hamid-Karzai - Rais Ashraf Ghani amekimbia na maelfu ya Waafghanistan wanatafuta kuondoka katika nvhi hiyo. Jumuiya ya kimataifa, kwa upande wake, inaangalia matukio hayo kwa wasiwasi mkubwa, huku ikijaribu kuandaa zoezi la uokoaji kwa raia wa kigeni vnchini Afghanistan.

Kutokana na hali hii "mbaya sana" kulingana na maneno ya ikulu ya Elysée, Emmanuel Macron amelihutubia taifa, Jumatatu hii, Agosti 16, kutoka Fort Brégançon, huko Bormes-les-Mimosas (Var), ambapo yuko likizo. Kabla ya kulihutubia taifa, Rais wa Jamhuri alizungumza saa sita mchana katika kikao cha Baraza la Ulinzi kupitia nia ya video, ambapo Waziri wa Mambo ya nje, Jean-Yves Le Drian na Waziri wa Jeshi, Florence Parlywameshiriki.

"Mabadiliko ya kihistoria yanatazamiwa kufanywa nchini Afghanistan,ikiwa ni pamoja na athari kubwa kwa jamii nzima ya kimataifa", ametangaza Emmanuel Macron, kwa sababu "baada ya vita vya miaka ishirini, baada ya uamuzi wa kurudisha majeshi ya Marekani (. ..), Kabul imeanguka mikononi mwa Wataliban katika masaa machache ”. Hapo hapo, "hali inazidi kuzorota haraka", hali ambayo "inahitaji maamuzi na mipango ya haraka".

“Udharura wa kwelini kuhakikisha usalama  wa wananchi wenzetu. Lazima wote waondoke nchini, na vile vile Waafghanitan waliofanya kazi kwa niaba ya Ufaransa, ”amebaini rais wa Ufaransa. Zoezi la uokoaji tayari limeanza katika wiki zilizopita. "Wafanyikazi wote wa Afghanistan

waliotumikia Ufaransa na familia zao tayari wamepokelewa nchini Ufaransa," ameongeza.

Hata hivyo, Emmanuel Macron almeamua kutuma "ndege mbili za kijeshi za vikosi vyetu maalum" huko Afghanistan. Watakuwa "huko kwa masaa machache". Emmanuel Macron anasisitiza kuwa jamii ya kimataifa itazungumza kwa sauti moja na kuungana hivi karibuni, ili Afghanistan isiwe tena "mahali pa ugaidi".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.