Pata taarifa kuu
MAREKANI-USALAMA

Pentagon: Marekani yatakiwa kutoa ulinzi katika uwanja wa ndege wa Kabul

Jeshi la Marekani linashirikiana na wanajeshi wa Uturuki na wale kutoka nchi zingine kuondoa watu ambao wamekusanyika katika uwanja huo ili kuruhusu ndege za kurudi tena kufaya safari ya kuwahamisha raia wanaohofia usalama wao, msemaji wa Wizara ay Ulinzi amesema Jumatatu wiki hii.

Msemaji wa Pentagon John Kirby wakati wa mkutano kuhusu hali nchini Afghanistan, Washington, Agosti 12, 2021.
Msemaji wa Pentagon John Kirby wakati wa mkutano kuhusu hali nchini Afghanistan, Washington, Agosti 12, 2021. AP - Andrew Harnik
Matangazo ya kibiashara

Akiongea katika mkutano na waandishi wa habari, John Kirby amesema Waziri wa Ulinzi Lloyd Austin ameidhinisha kupelekwa kwa kikosi cha ziada kwa mji mkuu wa Afghanistan, ambapo idadi ya wanajeshi wa Marekani waliopewa jukumu la kulinda mchakato wa kuhamisha watu kutoka nchini Afghanistan itafikia karibu 6,000.

Kama tahadhari kutokana na hali ya usalama katika uwanja wa ndege, ambapo mamia ya Waafghanistan walikusanyika Jumapili, wakiwa na hamu ya kuondoka nchini kwa dharura kutokana na ushindi wa kijeshi wa waasi wa Taliban, safari za ndege za kwenda au kutoka Kabul zimesitishwa .

Kufikia sasa, msemaji wa Pentagon amesema, "watu mia kadhaa" wamesafirishwa kwa ndege kutoka Kabul.

John Kirby amesema zaidi ya wanajeshi 3,000 wa Marekani wanaweza kupelekwa Jumanne katika mji mkuu wa Afghanistan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.