Pata taarifa kuu
ALBANIA

Albania kuwapokea wakimbizi wa Afghanistan

Albania imejibu vyema ombi la Washington la kuwapokea kwa muda wakimbizi wa Afghanistan wanaotafuta visa za kuingia Marekani, Waziri Mkuu Edi Rama amesema Jumapili hii wakati vikosi vya Taliban vikiingia k katika mji mkuu wa Afghanistan, Kabul.

Mapiano kati ya Taliban na vikosi vya serikali ya Afghanistan yasababisha mamia ya maelfu watu kuyahama makaazi yao.
Mapiano kati ya Taliban na vikosi vya serikali ya Afghanistan yasababisha mamia ya maelfu watu kuyahama makaazi yao. AP - Sidiqullah Khan
Matangazo ya kibiashara

Edi Rama amebaini kwamba utawala wa rais Joe Biden hivi karibuni uliomba Albania, ambayo ni mwanachama wa NATO, ikiwa inaweza kutumika kama nchi pokezi kwa wakimbizi wa Afghanistan ambao wanaelekea nchini Marekani.

"Hatungeweza kusema" hapana ", sio tu kwa sababu washirika wetu wakuu wanatuomba, lakini kwa sababu sisi ni Albania," ameandika Edi Rama kwenye ukurasa wake wa Facebook.

Wiki iliyopita vyanzo kadhaa viliambia shirika la habari la Reuters kwamba utawala wa Biden umekuwa na majadiliano juu ya suala hili na nchi kama Kosovo na Albania.

Huko Kosovo, Luan Dalipi, mkurugenzi mkuu wa ofisi ya Waziri Mkuu Albin Kurti, amesema serikali yake imekuwa ikiwasiliana na mamlaka ya Marekani kuwapokea wakimbizi wa Afghanistan tangu katikati ya mwzi Julai.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.