Pata taarifa kuu

Prague yashikilia hatua ya kuwafurusha wakimbizi wa Afghanistan

Jamhuri ya Czech itaendeleza zoezi la kuwarejesha nyumbani wakimbizi kutoka Afghanistan licha ya kuzorota kwa hali ya usalama nchini Afghanistan, Waziri wa Mambo ya Ndani wa Jamhuri ya Czech Jan Hamacek amesema Ijumaa wiki hii.

Baadhi ya nchi za Umoja wa Ulaya, pamoja na Ufaransa, Denmark na Ujerumani tayari zimetangaza kusitisha hatua ya kuwafukuza wakimbizi kutoka Afghanistan kwa sababu ya kuzorota kwa usalama.
Baadhi ya nchi za Umoja wa Ulaya, pamoja na Ufaransa, Denmark na Ujerumani tayari zimetangaza kusitisha hatua ya kuwafukuza wakimbizi kutoka Afghanistan kwa sababu ya kuzorota kwa usalama. - AFP
Matangazo ya kibiashara

"Jamhuri ya Czech inashughulikia kila ombi la mkimbizi anayetaka hifadhi kibinafsi, inachunguza kwa uangalifu sababu ili kuamua ikiwa (ombi) hilo limekubaliwa au la. Tutafanya uchunguzi kwa kila mkimbizi aliyeomba hifadhi nchini hapa," waziri huyo ameiambia tovuti ya habari http: // www.idnes .cz

Baadhi ya nchi za Umoja wa Ulaya, pamoja na Ufaransa, Denmark na Ujerumani tayari zimetangaza kusitisha hatua ya kuwafukuza wakimbizi kutoka Afghanistan kwa sababu ya kuzorota kwa usalama.

Wakati huo huo kundi la Taliban limeteka miji mikubwa zaidi Ijumaa, huku likielekea kwenye udhibiti kamili wa Afghanistan na kuzidi kuusogelea mji mkuu Kabul, wakati Marekani na Uingereza zikituma wanajeshi kuondoa raia wao Kabul.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.