Pata taarifa kuu
UJERUMANI

Berlin yatuma ndege aina ya A400M kwenda Kabul kuondoa wafanyakazi wa ubolozi

Jeshi la Ujerumani litatuma ndege za usafirishaji za A400M na wanaanga 30 ndani ya ndege hiyo katika mji wa Kabul kuwahamisha wafanyakazi wa ubalozi na raia wa Afghanistan walioshirikiana nao wakati Taliban iinauzingira mji mkuu huyo wa Afghanistan, limeripoti gazeti la Bild am Sonntag.

Makao makuu ya Bunge la Ujerumani,Bundestag, huko Berlin.
Makao makuu ya Bunge la Ujerumani,Bundestag, huko Berlin. REUTERS/Stefanie Loos
Matangazo ya kibiashara

Gazeti la Jumapili linataja vyanzo visivyojulikana kuwa ndege hizo zitatua katika mji wa nchi jirani, labda mji mkuu wa Uzbek Tashkent.

Msemaji wa Wizara ya Ulinzi amesema ujumbe wa uokoaji uliandaliwa usiku, lakini amekataa kutoa maoni zaidi kuhusu habari za gazeti hilo.

Taliban iliingia katika mji wa Kabul Jumapili wakati Marekani imekuwa ikiwaondoa wanadiplomasia wake kutoka majengo ya ubalozi wake kwa helikopta, na waziri wa serikali ya Afghanistan amesema serikali itakabidhiwa utawala wa mpito.

Idhini ya bunge la Ujerumani, inayohitajika kwa operesheni kama hiyo ya kijeshi, inaweza kutolewa baada ya ukweli kutokana na udharura wa ujumbe huu, kulingana na Gazeti la Jumapili la Bild.

Siku ya Jumamosi serikali ilisema kwamba jeshi lilikuwa likijiandaa kuwaondoa wafanyakazi wa ubalozi katika mji wa Kabul na kubaini kwamba zoezi hilo litaidhinishwa na Bunge.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.