Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Afghanistan: London na Washington zatuma wanajeshi kuwaondoa raia wao

Uingereza na Marekani zinaandaa zoezi la kuwaondoa raia wao na raia wa Afghanistan waliofanya kazi kwa niaba ya nchi hizo nchini Afghanistan kutokana na kusonga mbele kwa Taliban. Nchi hizi mbili zitatuma vikosi vya ziada kutokana na hali hiyo.

Msemaji wa Pentagon John Kirby wakati wa mkutano kuhusu hali inayoendelea nchini Afghanistan, Washington, Agosti 12, 2021.
Msemaji wa Pentagon John Kirby wakati wa mkutano kuhusu hali inayoendelea nchini Afghanistan, Washington, Agosti 12, 2021. AP - Andrew Harnik
Matangazo ya kibiashara

Wanajeshi kutoka nchi hizi mbili wanatarajiwa kuanza kuwasili nchini Afghanistan siku chache zijazo. Uingereza itatuma wanajeshi 600. Lakini hawaji kushiriki katika mapigano. "Usalama wa raia wa Uingereza, wanajeshi wa Uingereza na wafanyakazi wa zamani wa Afghanistan ndio kipaumbele chetu cha kwanza," Waziri wa Ulinzi amesema huko London Alhamisi hii Agosti 12. Dhamira yao itakuwa kuhakikisha usalama wa ubalozi huko Kabul na kuhamishwa kwa raia wa Afghanistan ambao wameisaidia Uingereza.

Marekani, kwa upande wake, itatuma wanajeshi 3,000 kurudi Afghanistan, na hivyo kutia nguvu uwepo wao wa kijeshi ingawa wengi wameondoka nchini humo. Lakini kwa upande Washington pia, hatua hii inakusudia kuhakikisha zoezi la kuaondoa raia wake linakwenda salama.

"Tunaamini hili ndilo jambo la busara zaidi kufanya kutokana na hali ya usalama kuzorota kwa kasi karibu na mji wa Kabul. Nasisitiza kwamba wanajeshi hawa watapelekwa kwa ombi la Wizara ya Ulinzi kuhakikisha usalama na mwenendo mzuri katika zoezi la kuwaondoa wafanyikazi wetu wa kiraia, na kuwezesha na kuharakisha kushughulikia maombi maalum ya visa. Ni zoezi la muda na lenye lengo maalum. Shambulio lolote dhidi ya vikosi hivi litasababisha ulipizaji kisasi, ”amesema John Kirby, msemaji wa Pentagon.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.