Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Mashirika ya habari-Afghanistan: Taliban waanza kuingia Kabul

Mashambulio hayo ya waasi yanafanyika kutoka pande zote, linaripoti shirika la habari la Reuters, ikinukuu Wizara ya Mambo ya Ndani ya Afghanistan. Taliban wanaamuru wapiganaji wao, shirika hilo limesema, kuepuka vurugu katika mji mkuu na kuwaruhusu wale wanaotaka kuondoka kwenda.

Jumapili hii, Agosti 15, Taliban sasa wanadhibiti mikoa mingi ya Afghanistan. Unabaki tu mji wa Kabul tambao uko mikononi mwa mamlaka ya nchi.
Jumapili hii, Agosti 15, Taliban sasa wanadhibiti mikoa mingi ya Afghanistan. Unabaki tu mji wa Kabul tambao uko mikononi mwa mamlaka ya nchi. AFP - ROBERTO SCHMIDT
Matangazo ya kibiashara

Wakati huo huo wapiganaji wa Taliban wametwaa udhibiti wa mji a Nangarhar Jumapili, Agosti 15, 2021. Waasi wamechukua udhibiti wa Jalalabad bila upinzano wowote, na hivyo kuhakikisha upatikanaji wa barabara zinazoongoza kwa nchi jirani ya Pakistan. Kabul ni jiji kuu la mwisho ambalo bado halijadhibitiwa na Taliban.

Kama miji mingine mikuu zaidi ya ishirini ya mikoa, Jalalabad, jiji kubwa mashariki mwa Afghanistan, sasa liko chini ya udhibiti wa Taliban. “Tumeamka asubuhi ya leo tukiona bendera nyeupe za Taliban kote mjni. Wako mjini. Waliingia bila upinzani, "mkazi mmoja ameliambia shiria la habari la AFP . "Kuruhusu kuingia kwa Taliban ilikuwa njia pekee ya kuokoa maisha ya raia," afisa wa Afghanistan huko aameliambia shirika la habari la Reuters.

Waasi wamethibitisha habari hiyo: “Dakika chache zilizopita, Mujahedin wameingia Jalalabad, mji mkuu wa mkoa wa Nangarhar. Maeneo yote sasa yako chini ya udhibiti wao, ”msemaji wa Taliban Zabihullah Mujahid amesema leo Jumapili. Saa chache mapema, waasi walitwaa udhibiti wa mji mkubwa wa kaskazini mwa Afghanistan, Mazar-i-Sharif. Baada ya Kandahar na  Herat,hapo kabla.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.