Pata taarifa kuu
MAREKANI

Marekani yatafuta nchi zilizo tayari kuwapokea wakimbizi wa Afghanistan

Utawala wa Marekani umefanya mazungumzo ya siri na nchi kadhaa katika jaribio la kupata mikataba ya kuwapokea kwa muda wakimbizi wa Afghanistan ambao walifanya kazi kwa niaba ya serikali ya Marekani, maafisa wanne wa wamesema wakinukuliwa shirikala habari la Reuters.

raia waAfghanistan wakiyatoroka makaazi yao kufuatia mapigano katika mji wa Herat, Jumapili Agosti 8, 2021.
raia waAfghanistan wakiyatoroka makaazi yao kufuatia mapigano katika mji wa Herat, Jumapili Agosti 8, 2021. AP - Hamed Sarfarazi
Matangazo ya kibiashara

Nchi kama Kosovo na Albania zimeshirika katika mazungumzo hayo na zimebaini nia ya utawala wa Biden kulinda Waafghanistan waliokuwa wakifanya kazi na Marekani kutokana na ulipizaji kisasi cha Taliban.

Wakati Taliban inaendelea kusonga mbele kwa kasi kubwa katika maeneo mbalimbali nchini Afghanistan, Marekani ilitangaza siku ya Alhamisi kwamba itatuma maafisa 1,000 nchini Qatar ili kuharakisha zoezi la kushughulikia maombi maalum ya wahamiaji (SIV).

Waafghanistan ambao wamewahi kuwa wakalimani kwa serikali ya Marekani wanaweza kuomba SIV.

Kufikia sasa, karibu Waafghanistan 1,200 wamehamishwa kwenda Marekani na idadi hii inatarajiwa kuongezeka hadi 3,500 katika wiki zijazo kama sehemu ya Operesheni ya "Wakimbizi Washirika".

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.