Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Afghanistan: mji wa Lashkar Gah waanguka mikononi mwa Taliban

Taliban wamefanikiwa kuchukua udhibiti wa karibu nusu ya miji mikuu ya mikoa wa nchi hiyo. Miji mikubwa mitatu bado iko chini ya udhibiti wa serikali.

Taliban walikuwa wamedai usiku kuiteka miji ya Kandahar (Kusini), jiji la pili kwa ukubwa nchini, habari iliyothibitishwa na mkaazi mmoja wa mji huo. Pia siku ya Alhamisi walichukuwa udhibiti wa mji wa Herat (Magharibi), mji wa tatu kwa ukubwa nchini Afghanistan.
Taliban walikuwa wamedai usiku kuiteka miji ya Kandahar (Kusini), jiji la pili kwa ukubwa nchini, habari iliyothibitishwa na mkaazi mmoja wa mji huo. Pia siku ya Alhamisi walichukuwa udhibiti wa mji wa Herat (Magharibi), mji wa tatu kwa ukubwa nchini Afghanistan. JAVED TANVEER AFP
Matangazo ya kibiashara

Lashkar Gah, mji mkuu wa mkoa wa Helmand kusini mwa Afghanistan, umetekwa na Taliban Ijumaa hii (Agosti 13). “Wakaazi wa mji wa Lashkar Gah wamelazimika kuyatoroka makaazi yao. Waliamua kusitisha mapigano kwa saa 48 ili kuwaondoa "wanajeshi na maafisa wa kiraia, afisa mwandamizi wa usalama ameliiambia ameliambia shirika la habari la AFP. Taliban hapo awali walikuwa wamedai kuutekwa mji huo.

Taliban pia ilichukua bila upinzani wowote leo  Ijumaa asubuhi mji wa Chaghcharan, mji mkuu wa mkoa wa kati wa Ghor, msemaji wa gavana Zalmai Karimi ameliiambia shirika la habari la AFP.

Taliban wachukuwa udhibiti wa miji ya Kandahar na Herat

Taliban walikuwa wamedai usiku kuiteka miji ya Kandahar (Kusini), jiji la pili kwa ukubwa nchini, habari iliyothibitishwa na mkaazi mmoja wa mji huo. Pia siku ya Alhamisi walichukuwa udhibiti wa mji wa Herat (Magharibi), mji wa tatu kwa ukubwa nchini Afghanistan, na walikuwa kwenye umbali wa kilomita 150 kutoka Kabul, pia wakidhibiti mji wa Ghazni, kusini magharibi mwa mji mkuu.

Katika siku nane, waliteka karibu nusu ya miji mikuu ya mikoa ya Afghanistan. Wanadhibiti sehemu nyingi za kaskazini, magharibi na kusini mwa nchi. Kabul, Mazâr-e Charîf, jiji kuu kaskazini, na Jalalabad (mashariki) ndio miji mikubwa mitatu tu ambayo bado iko chini ya udhibiti wa serikali.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.