Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Ujerumani yatoa wito kwa raia wake kuondoka Afghanistan

Ujerumani imewataka raia wake kuondoka Afghanistan haraka iwezekanavyo kutokana na kuzorota kwa hali ya usalama nchini humo.

UJerumani imewataka raia wake kuondoka haraka Afghanistan.
UJerumani imewataka raia wake kuondoka haraka Afghanistan. AFP
Matangazo ya kibiashara

"Raia wa Ujerumani wanatakiwa kuondoka nchini Afhanistan kwa ndege zilizopangwa haraka iwezekanavyo," wizara ya mambo ya nje imesema katika taarifa iliyochapishwa kwenye wavuti yake.

Siku ya Jumatatu Waziri wa ulinzi wa Ujerumani alikataa wito wa Berlin wa kutuma wanajeshi nchini Afghanistan baada ya waasi wa Taliban kuchukua udhibiti wa mji wa Kunduz, mji ambao wanajeshi wa Ujerumani wametumwa kwa karibu miaka kumi.

Alhamisi wiki hii Taliban wameteka mji wa Ghazni, kilomita 150 kusini magharibi mwa Kabul, baada ya mapigano makali, ambayo yanaweza kuwaruhusu kuendelea kusonga mbele kuelekea Kabul, mji mkuu.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.