Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Afghanistan:Taliban yadhibiti Ghazni, mji wa kimkakati

Taliban wameteka Alhamisi hii mji wa kimkakati wa Ghazni, kilomita 150 kusini magharibi mwa mji mkuu wa Afghanistan, Kabul. Ghazni ni mji mkuu wa mkoa wa kumi kuingia mikononi mwa Taliban kwa wiki moja, habari ya kutekwa kwa mji huo na Taliban imethibitrishwa na mshauri wa mamlaka ya mkoa.

Vikosi vya jeshi la Afghanistan karibu na Ghazni, Novemba 29, 2020 (picha ya kumbukumbu).
Vikosi vya jeshi la Afghanistan karibu na Ghazni, Novemba 29, 2020 (picha ya kumbukumbu). REUTERS - MUSTAFA ANDALEB
Matangazo ya kibiashara

"Ninaweza kudhibitisha kuwa mji wa Ghazni uko mikononi mwa Taliban tangu leo asubuhi (Alhamisi). Wamechukua udhibiti wa maeneo muhimu ya jiji: ofisi ya gavana, makao makuu ya polisi na gereza," Nasir Ahmad Faqiri, mkuu wa Halmashauri ya Mkoa wa Ghazni ameliambia shirika la habari la AFP.

Amesema mapigano bado yanaendelea katika sehemu za jiji, lakini Taliban wamedhibiti mji huo. Taliban pia wamedai kudhibiti mji wa Ghazni.

Ghazni ni mji mkuu wa mkoa ulio karibu na mji Kabul uliotekwa na waasi tangu walipoanzisha mashambulizi yao mwezi Mei baada ya kuanza kuondoka kwa majeshi ya kigeni, ambapo zoezi hilo litakamilika mwishoni mwa mwezi Agosti.

Taliban wamesonga mbele kwa kasi kubwa katika siku za hivi karibuni. Katika wiki moja, wamedhibiti miji mikuu 10 kati ya 34, ikiwa ni pamoja na saba iliyoko kaskazini mwa nchi, jimbo ambalo kila wakati ulikuwa ukiwapinga hapo zamani.

Ishara ya wasiwasi katika mji mkuu

Jumanne jioni, waliteka Pul-e-Khumri, mji mkuu wa mkoa wa Baghlan, kilomita 200 kaskazini mwa Kabul. Kwa hivyo wanakaribia mji mkuu kutoka kaskazini na kutoka kusini.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.