Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Afghanistan: Mapigano yaendelea kurindima karibu na mji mkuu Kabul

Taliban, ambao sasa wanadhibiti 65% ya nchi ya Afghanistan, wanatishia kuiteka miji mikuu ya mikoa kumi na moja na wanajaribu kuuzingira mji wa Kabul ili usiwezi kuata msaada wa vikosi vya serikali kutoka eneo la Kaskazini, afisa mwandamizi wa Umoja wa Ulaya amesema Jumanne.

Vikosi vya usalama vya Afghanistan katika mitaa ya Kabul Agosti 3, 2021.
Vikosi vya usalama vya Afghanistan katika mitaa ya Kabul Agosti 3, 2021. AP - Rahmat Gul
Matangazo ya kibiashara

Baada ya vikosi vya jeshi la Marekani kuondoka nchini humo, waasi Taliban walipata ushindi wa haraka katika uwanja wa vita katika wiki za hivi karibuni na kuimarisha udhibiti wao juu ya maeneo ambayo wameyateka kaskazini mwa Afghanistan, na kuwalazimisha wakazi kutoroka makaazi yao.

Wakati huo huo wameimarisha udhibiti wao baada ya kuuteka mji wa Aybak, mji mkuu wa jimbo la Samangan, kwenye barabara kuu kati ya Mazar-i-Sharif, jiji kubwa kaskazini mwa nchi, na Kabul, mji mkuu, kwa kushikilia majengo ya serikali, wakazi wamebaini.

Maafisa wengi wa vikosi vya usalama vya serikali vimeonekana vikijiondoa katika mji huo, wameongeza.

"Suluhisho pekee ni kujipanga au kutafuta njia ya kuondoka kwenda Kabul," Sher Sher Abbas, amesema afisa wa ushuru ambaye ni baba wa familia ya watu tisa.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.