Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Taliban yadhibiti miji mikuu mingine mitatu ya mikoa, ikiwa ni pamoja na Kunduz

Waasi wanaendelea kusonga mbele nchini Afghanistan. Mapigano makali yalmetokea mapema Jumapili hii, Agosti 8, kati ya jeshi la Afghanistan na wapiganaji wa Taliban, katikati mwa mji mkuu wa mkoa wa Kunduz. 

Wanajeshi wa Afghanistan huko Kunduz wakati wa mapigano na wanamgambo wa Taliban, hapa ilikuwa mwaka 2015.
Wanajeshi wa Afghanistan huko Kunduz wakati wa mapigano na wanamgambo wa Taliban, hapa ilikuwa mwaka 2015. Wakil KOHSAR AFP/File
Matangazo ya kibiashara

Mji wa Kunduz umeanguka mikononi mwa Taliban. Muda mfupi baadaye, Sar-e-Pul, kaskazini magharibi, pia ulianguka mikononi mwa kundi hilo, ikiwa ni pamoja na mji wa Taloqan, katika mkoa wa Takhar.

Video zinazoonyesha milipuko na magari kuteketea ka moto katikati mwa jiji la Kunduz zimekuwa zikisambaa kwenye mitandao ya kijamii tangu Jumapili asubuhi, mwandishi wetu huko Kabul, Sonia Ghezali, ameripoti. Karibu watu 300,000 wanaishi katika mji huo.

Taliban wamewaachilia huru wafungwa wengi. maafisa wa vikosi vya usalama vya Afghanistan wameripotiwa kukimbilia katika uwanja wa ndege. Mapigano bado yanaendelea huko Kunduz; uwanja wa ndege tu na kituo cha jeshi bado wanakabiliana na mashambulizi ya Taliban, kulingana na mbunge wa eneo hilo.

Maelfu ya familia wamelazimika kutoroka makaazi yao kwa sababu ya vurugu hizo. Wale ambao wamebaki wamekwama wakati jeshi la anga la Afghanistan likifanya mashambulizi ya anga.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.