Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Afghanistan: Mkuu wa mamlaka ya mawasiliano auawa

Mkuu wa mamlaka ya mawasiliano nchini Afghanistan ameuawa wakati wa sala ya Ijumaa huko Kabul, Wizara ya Mambo ya Ndani imesema, siku chache baada ya Taliban kuahidi kulenga maafisa wa serikali.

Maafisa wa vikosi vya usalama vya Afghanistan katika mitaa ya Kabul, Agosti 3, 2021.
Maafisa wa vikosi vya usalama vya Afghanistan katika mitaa ya Kabul, Agosti 3, 2021. AP - Rahmat Gul
Matangazo ya kibiashara

"Kwa bahati mbaya, magaidi katili wamefanya kitendo kingine cha kinyama na kumuua raia mzalendo wa Afghanistan ambaye amekuwa akipinga propaganda za adui (...), Dawa Khan Menapal, wakati wa sala ya Ijumaa" katika mji mkuu, msemaji wa Wizara ya Habari, Mirwais Stanikzai, amesema katika ujumbe wa WhatsApp kwa vyombo vya habari.

Hayo yanajiri wakati  viongozi wa nchi tano za Asia ya kati wanafanya mazungumzo nchini Turkmenistan leo Ijumaa, kuzungumzia juu ya kuongezeka kwa vita nchini Afghanistan baada ya vikosi vya kimataifa kuondoka nchini humo.

Mazungumzo hayo ya mjini Avaza yanafanyika katika wakati ambapo kundi la Taliban linapambana na vikosi vya serikali ya Afghanistan katika miji kadhaa ya nchi hiyo ikiwemo wilaya zinazopakana na mataifa matatu ya zamani ya Umoja wa Kisovieti -Tajikistan, Turkmenistan na Uzbekistan.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.