Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Mdororo wa usalama Afghanistan: Ashraf Ghani ashushia lawama Marekani

Rais wa Afghanistan Ashraf Ghani anasema kuanza kuzorota kwa usalama nchini mwake ni kwa sababu ya hatua ya Marekani kuamua kwa haraka kuondoa wanajeshi wake katika taifa hilo.

rais wa Afghanistan Ashraf Ghani mbeke ya Bunge huko Kabul, Oktoba 21, 2020.
rais wa Afghanistan Ashraf Ghani mbeke ya Bunge huko Kabul, Oktoba 21, 2020. AFP - WAKIL KOHSAR
Matangazo ya kibiashara

Rais Ghani amewaambia wabunge kuwa alikuwa ameuonya uongozi wa Marekani kuhusu athari ya kuondoa wanajeshi wake haraka katika taifa hilo kungekuwa na matokeo mabaya.

Siku ya Jumatatu, wanajeshi wa Afganistan wamekuwa wakipambana na kundi la Taliban, kuzuia miji ya Lashkar Gah, Kandahar na  Herat kudhibitiwa na kundi hilo, wakati huu maelfu ya watu wakiyakimbia makwao.

Tangu mwezi Mei, kundi la Taliban limeendeleza mashambulizi katika ngome ambazo hapo awali zilikuwa zinadhibitiwa na vikosi vya serikali na vile vya kigeni, baada ya Marekani na washirika wake wa jeshi la NATO, kutangaza kuwa vikosi vyake vitarejea nyumbani ifikapo tarehe 31 mwezi huu baada ya kuwa nchini humo kwa miaka 20.

Marekani imekuwa ikisema itaendelea kuwapa hifadhi maelfu ya raia wa nchi hiyo kwa sababu ya utovu wa usalama unaoendelea, huku Umoja wa Ulaya ukisema hautatambua serikali itakayoundwa na Taliban iwapo itatumia nguvu kuingia madarakani.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.