Pata taarifa kuu
AFGHANISTANI

Biden aidhinisha msaada wa dola milioni 100 kwa wakimbizi wa Afghanistan

Rais wa Marekani Joe Biden ameidhinisha kufunguliwa kwa mfuko wa dharura wa dola milioni 100 (euro 84.9 milioni) ili kukidhi mahitaji ya wakimbizi wa Afghanistan, Wite House imesema.

Afisa wa polisi katika kituo cha polisi karibu na mji mkuu wa Kabul, Julai 13, 2021.
Afisa wa polisi katika kituo cha polisi karibu na mji mkuu wa Kabul, Julai 13, 2021. REUTERS - MOHAMMAD ISMAIL
Matangazo ya kibiashara

Joe Biden pia ameidhinisha matumizi ya dola milioni 200 katika huduma na mali kutoka kwa hifadhi ya mashirika ya serikali ya Marekani.

Kulingana na taarifa kutoka hite House, Biden ametangaza uungwaji mkono wa Marekani kwa rais Afghanistan na raia wake, wakati mashambulizi ya Taliban yanaweka shinikizo kwa serikali ya Afghaistan.

Wakati wa mazungumzo kwa njia ya simu, Joe Biden na Ashraf Ghani wamekubaliana kuwa "mashambulizi ya Taliban ni kinyume na taarifa za kundi hilo ambalo liliahidi kuunga mazunumzo ili kupata suluhu ya mgogoroo", imeelezwa katika taarifa iliyotolewa na White House.

Joe Biden alitangaza mwisho wa ujumbe wa kijeshi nchini Afghanistan, Agosti 31.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.