Pata taarifa kuu
AFGHANISTAN-USALAMA

Kamanda wa vikosi vya Marekani Afghanistan kuachia ngazi

Kamanda wa wanajeshi wa Marekani nchini Afghanistan, Jenerali Austin Miller, anatarajia kuachia ngazi kwenye nafasi yake lleo Jumatatu, maafisa wa Marekani wamebaini, na hivyo kusitisha mgogoro mrefu zaidi wa nje wa Marekani wakati Taliban wakiendelea na mashambulio yao nchini humo.

Jenerali Austin Miller, (kushoto) akiwa pamoja na Jenerali Kenneth McKenzie, (kulia), kwenye moja ya sherehe huko Kabul, wakati Miller akitangaza kuachilia ngazi kama mkuu wa vikosi vya Marekani Afghanistani, Julai 12, 2021.
Jenerali Austin Miller, (kushoto) akiwa pamoja na Jenerali Kenneth McKenzie, (kulia), kwenye moja ya sherehe huko Kabul, wakati Miller akitangaza kuachilia ngazi kama mkuu wa vikosi vya Marekani Afghanistani, Julai 12, 2021. REUTERS - PHIL STEWART
Matangazo ya kibiashara

Sherehe imepangwa huko Kabul kuashiria kumalizika rasmi kwa ujumbe wa Marekani nchini Afghanistan, ambao tarehe ya mwisho imewekwa Agosti 31 na Rais Joe Biden.

Jenerali Kenneth McKenzie, mkuu wa vikosi vya Marekani katika maeneo ya mizozo kama Afghanistan, Iraq na Syria, amezuru mji wa Kabul kuonyesha mshikamano na vikosi vya usalama vya Afghanistan na kuwahakikishia kuwa Marekani itaendelea kuwasaidia.

Leo Jumatatu, wapiganaji wa Taliban wamezingira mji wa Ghazni katikati mwa Afghanistan.

"Hali katika mji wa Ghazni ni mbaya sana (...) Wataliban wanatumia nyumba za raia kama mahali pa kujificha na wanarushia risasi vikosi vya ANDSF (vikosi vya usalama vya Afghanistan), hali ambayo inatatiza vikosi hivyo kujibu, amebaini Hassan Rezayi mmaja wa wajumbe wa Halmashauri ya mji wa Ghazni.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.