Pata taarifa kuu
AFGHANISTANI

Balozi za Marekani na Uingereza zashutumu Taliban kwa "mauaji" ya raia

"Mauaji" ya raia yanayotekelezwa na Taliban yameripotiwa katika baadhi ya wilaya, balozi za Marekani na Uingereza zimebaini katika taarifa Taliban ikiendelea kushikiliwa udhibiti katika miji mitatu mikubwa ya nchi hiyo, Herat, Kandahar na Lashkar Gah ambapo mapigano yanaendelea kurindima.

Maafisa wa idara za usalama wa Afghanistan kwenye eneo la mlipuko wa gari huko Kandahar, Julai 4, 2021.
Maafisa wa idara za usalama wa Afghanistan kwenye eneo la mlipuko wa gari huko Kandahar, Julai 4, 2021. AFP - JAVED TANVEER
Matangazo ya kibiashara

Tangu kuanza kwa zoezi la kuondoka kwa wanajeshi wa kigeni nchini Afghanistan, ambalo litakamilika mwishoni mwa mwezi Agosti, Taliban wameanzisha mashambulizi makubwa dhidi ya vikosi vya serikali na wamechukua maeneo makubwa ya nchi. Maelfu ya Waafghani wametoroka makazi yao na kukimbilia maeneo salama katika vijiji jirani au katika miji mikuu ya mkoa.

Raia wanakabiliwa na hali ngumu, huku mauaji ya raia yakiripotiwa katika baadhi ya wilaya, balozi za Marekani na Uingereza zmebaini.

Kulingana na vyanzo mbalimbali kundi la Wanamgambo wa Taliban linakaribia kuukamata mji mkuu wa jimbo la Helmand, kusini mwa Afghanistan baada ya mapigano ya siku kadhaa yaliyoshuhudia wanamgambo wakichukua udhibiti wa wilaya muhimu za mji huo.

Duru zimearifu kulikuwa na mapambano makali Jumatatu wiki hii baina ya wapiganaji wa Taliban na jeshi la Afghanistan lakini wanamgambo wanasonga mbele licha ya mashambulizi ya anga na operesheni ya makomando wa vikosi vya serikali.

Iwapo kundi hilo litafanikiwa kuukamata mji mkuu wa jimbo la Helmand, kusini mwa Afghanistan itakuwa ni mara ya kwanza tangu mwaka 2016 kwa wapiganaji wake kudhibiti mji mkuu wa jimbo ndani ya nchi hiyo.

Kusambaza :
Ukurasa haipatikani

Maudhui unayojaribu kuyatafuta hayapatikani kwa sasa au yamekwishaondolewa.